Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge leo amefanya
ziara katika masoko na mitaa ya manispaa
ya Singida ili kubaini hali halisi ya
maeneo hayo na changamoto zinazowakabili
wafanya biashara wadogo maarufu
kama wamachinga.
Ziara hiyo iliyoshirikisha Kamati ya Usalama ya mkoa na
viongozi mbalimbali wa manispaa hiyo ililenga kubaini maeneo yenye changamoto
kwa wafanya biashara wenye maduka na wanaopanga bidhaa barabarani.
Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amewataka wakurungezi na wakuu wa wilaya kuhakikisha
zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara hao linafanyika kwa njia ya majadiliano
badala ya kutumia nguvu.
Aidha Dkt. Mahenge amemshauri Mkurungezi wa Manispaa ya
Singida mjini ashirikiane na vyombo vingine ikiwemo TARURA ili walete mapendekezo ya maeneo tarajiwa
pamoja na mipango ya namna ya utekelezaji.
Hata hivyo amebainisha kwamba maeneo tarajiwa lazima
yaandaliwe vizuri ikiwemo ujenzi wa vyoo, uwepo wa umeme na maji ili maeneo
hayo yawavutie wafanyabiashara.
Aidha amesema mchakato wa kubaini maeneo mapya ya kufanyia
biashara na mipango ya kufunga baadhi ya Barabara kwa nyakati tofauti inafanyika ili kuhakikisha kila mfanya
biashara anaendelea na shughuli zake bila kubughuziwa.
“Nashauri wafanyabiashara wa mjini ambao watatakiwa kupisha
maeneo waliopo watafutiwe mengine upande wa huko mjini na wafanyabiashara wa mitaani
watafutiwe maeneo karibu na mitaa yao.”
alisema Dkt. Mahenge
Hata hivyo amewataka wataalamu
mbalimbali waliofuatana nao kutumia fursa hiyo kufanya mipango miji wakati wa
kufungua maeneo mapya kwa ajili ya biashara.
Ametoa wito kwa wakurugenzi na wakuu wa wilaya kushirikiana
ili kuhakikisha zoezi la kuwapanga wafanyabiashara hao halichukui muda mrefu iwe
wameshapatiwa maeneo mapya ya bishara kwa njia ya majadiliano.
Ziara hiyo ilifanyika katika kata ya Ipembe barabara Nyerere,
Lumumba, sokoni na Posta ambapo kata ya majengo ilifanyika ziara barabara ya usafirishaji,
Ukombozi na Kituo cha mabasi cha zamani.
Wakati kata ya mandewa
ilifanyika maeneo ya Ginnery kuelekea hospitali ya manispaa.
Dkt. Binilithi Mahenge akiwa katika ziara kwenye soko la Kariakoo manispaa ya Singida mjini kuangalia changamoto na kero za wamachinga
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi Dorothy Mwaluko (aliyeshika kitambaa) akitoa ufafanuzi kwenye baadhi ya mambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bi Sophia Kizigo (kulia ) akijadili jambo na Mkurugenzi mtendajia Halmashauri hiyo Bi Asia Juma Messos wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa iliyofanyika katika Kata tatu za manispaa ya Singida mjijni
No comments:
Post a Comment