Akiongea leo wakati wa mapokezi ya
Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema kiasi
hicho cha fedha kimetumika katika miradi 55 ya maendeleo katika Mkoa mzima.
“Jumla ya miradi 55 inayohusu
TEHAMA, Elimu Afya, mazingira maji biashara, barabara programu za rushwa, VVVU/UKIMWI,
malaria na mapambano dhidi ya dawa za kulevya itatembelewa” amesema Mhe. Mahenge.
Amesema katika mbio hizo za Mwenge wa
Uhuru miradi mipya 9 itazinduliwa, miradi
miwili itafanyiwa ufunguzi, sita itawekwa jiwe la msingi na 36
itakaguliwa na miradi miwili itatembelewa.
Aidha Mhe. Mkuu wa mkoa amebainisha
kwamba kiasi hicho cha fedha kwenye miradi hiyo inatokana na michango ya
wananchi kiasi cha sh.Bilioni 1.9, mchango wa Halmashauri kiasi cha sh.milioni
69.6 na kiasi cha sh. milioni 4.6 kutoka Serikali kuu.
Hata hivyo Mhe. Dkt. Mahenge ametoa
wito kwa wanasingida wote kutumia kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2021 “TEHAMA ni
msingi wa Taifa endelevu” kwa kuwajibika ili kuleta maendeleo ya mtu na Taifa
kwa ujumla.
Amesema kutokana na umuhimu wa TEHAMA katika maendeleo ya Taifa mkoa umeendelea kusimamia zaidi ya mifumo 30 inayotumika katika mamlaka za Serikali za mitaa, Sekretarieti ya mkoa pamoja na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewataka
wananchi wa Singida kujiunga na bima ya afya ili kukabiliana na gharama za matibabu.
Amewasihi wananchi kutumia lishe
bora kwa afya imara ambapo kiwango cha udumavu kimeendelea kupungua hadi
kufikia asilimia 29 mwaka 2018.
Mkoa umeendelea kutafuta suluhisho
la tatizo la ukondefu na upungufu wa uzito kwa watoto kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa lishe ambapo jumla ya vituo 99 vya huduma
ya afya vinavyotoa matibabu kwa watoto
vimeanzishwa. Alibainisha mkuu wa
mkoa
Matukio mbalimbali katika picha
Mwenge wa Uhuru 2021, katika Mkoa wa Singida utakimbizwa kwa muda wa siku Tano (5), katika Wilaya Tano kwa kuanzia na Wilaya ya Iramba leo tarehe 20/07/2021 na utahitimisha mbio zake mnamo tarehe 24/07/2021 na tarehe 25/07/2021 utakabidhiwa Mkoa wa Dodoma.
MWENGE WA UHURU 2021 WAPOKELEWA MKOANI SINGIDA, MIRADI 55 KUZINDULIWA
No comments:
Post a Comment