MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
WAKATI WA MBIO MAALUM ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA YA SINGIDA JULAI 22, 2021 MKOANI SINGIDA
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Singida vijiji (kulia) Rashid Mohammed Mandoa akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mheshimiwa Ramadhan Ighondo (kulia) akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi akikagua mradi wa jengo ofisi ya mthibiti ubora wa shule katika Manispaa ya Singida wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Julai 22,2021
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi akizindua mradi wa jengo ofisi ya mthibiti ubora wa shule katika Manispaa ya Singida wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Julai 22,2021
Mapambano dhidi ya Malaria, chini ya kauli mbiu "Ziro Malaria Inaanza na Mimi nchukua hatua kuitokomeza".
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi akizungumza na clab ya wapinga Rushwa katika shule ya sekondari Mwenge iliyopo Manispaa ya Singida mara baada ya kutembelea na kujionea mapambano ya Rushwa
"KUPAMBANA NA RUSHWA NI JUKUMU LANGU, VUNJA UKIMYA TOA TAARIFA DHIDI YA VITENDO VYA RUSHWA, EPUKA KUSHIRIKI VITENDO VYA RUSHWA, SHIRIKI KUTOA USHAHIDI KUPAMBANA NA KUPINGA RUSHWA".
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mheshimiwa Ramadhan Ighondo akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Singida wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021
Mwenge wa Uhuru 2021 ukiwa Unawaka, Unang'ara na Kumelemeta ndani ya Wilaya ya Singida katika Miradi mbalimbali ya maendeleo
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tukio la uzinduzi wa mradi wa maji uliotumia kiasi cha Shilingi za kitanzania Milioni 4.5 na ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Singida pamoja na wataalam RUWASA mkoa Singida kusimamia mradi huo hadi kukamilika vizuri ili kuondoa adha waliyokuwa wakiipata wananchi wa kijiji cha Mughamo Manispaa ya Singida
Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Singida wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Maji wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 katika kijiji cha Mughamo Manispaa ya Singida. Mradi huo umezinduliwa na Kiongozi wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi Julai 22, 2021
Afisa TEHAMA Bw. Joseph Micka Joseph amezitaja baadhi ya mifumo inayotumika kuwa ni mfumo wa bajeti (Planrep), mfumo wa taarifa za Watumishi na Mishahara (Lowson –HCMIS), ukusanyaji wa mapato (LGRCIS), utunzaji wa taarifa za wagojwa (GoT- HoMIS) mfumo wa kiuhasibu katika utoaji wa huduma (FFRS), Taarifa za shule (SIS) mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi ( SAFARI), mfumo wa malipo (EPICOR- MUSE) na mfumo wa barua pepe.
Burudani mbalimbali zikiendelea wakati wa sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi (kulia) akisomewa taarifa fupi ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya kutoka kwa askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida Rajabu, alipotembelea banda la Polisi wakati wa sherehe za Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Fadhila Saimoni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Itaja kwa niaba ya wanafunzi wengine ameshukuru kwa ujio wa Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru kuzindua mradi wa Maji shuleni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (kushoto) akisherekea pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru (kulia) wakati wa sherehe za Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Sherehe za Mwenge wa Uhuru zikiendelea katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi (kulia) akikagua risala ya utii ya Wananchi wa Wilaya ya Singida kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (kushoto) wakati wa sherehe za Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi (kulia) akipokea risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili wakati wa sherehe za Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
Kwa upande mwingine Mwenge wa Uhuru 2021 katika Wilaya ya Singida umezindua mradi wa lishe bora katika kata ya Ilongero ambapo wilaya imejivunia kupunguza idadi ya watoto wenye utapiamlo kutoka watoto 22,854 kwa mwaka 2019/2020 hadi kufikia 18,215 mwaka 2021 kwa watoto chini ya miaka 5.
Aidha Afisa lishe wa mradi huo Bi. Asha Mahami amesisitiza kwamba uhamasishaji wa matumizi ya lishe bora yamefanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano 20 na vikao 32 vya wazazi na walezi katika vijiji na mitaa 61 na kata 31, lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto anapata lishe bora kwa siku 1,000 za mwanzo.
Aidha miradi mingine ni malaria uliopo kata ya Mtinko mradi wa maji katika shule ya sekondari ya Itaja, ujenzi wa tenk la maji , Maabara na jengo la uthibiti wa ubora wa elimu lililopo Manispaa ya Singida.
Kwa habari zaidi bonyeza; www.singida.go.tz
No comments:
Post a Comment