Wednesday, January 09, 2019

WAZIRI JENISTA MHAGAMA, AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA RAIS KUHUSU KIKOKOTOO CHA MAFAO YA WASTAAFU, MKOANI SINGIDA


Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. JENISTA MHAGAMA, jana Januari 09,2019 ameanza ziara ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu ambapo ameahidi kuchukua hatua kali kwa watumishi ambao watashindwa kutekeleza agizo hilo.

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo mapema jana alipokuwa mkoani Singida baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii - NSSF- na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma – PSSSF.

Waziri Mhagama amesema, matarajio katika utekelezaji wa maagizo hayo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais, ni kuwa na matokeo au mabadiliko makubwa yanayokusudiwa na kuonekana mapema iwezekanavyo ili malengo yaliyowekwa katika kipindi hiki yafikiwe mapema. Hivyo amewataka watendaji wa mifuko hiyo kubadilika na kutekeleza maagizo hayo.

“Kwa hiyo ndugu zangu watendaji, kila mmoja kwa nafasi yake atekeleze maagizo haya kwa ufanisi unaotarajiwa. Kama mtendaji atajikagua na kubaini kuwa atashindwa kwenda na kasi ya kutekeleza maagizo haya ya Rais, ni vizuri akajiondoa mapema” amesema Mheshimiwa Waziri Mhagama.

Akizungumzia kuhusu ziara yake, Mheshimiwa Waziri Mhagama amesema, lengo ni kukagua utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli Desemba 28, 2018 ili kujionea kama yameanza kutekelezwa kwa ufanisi nchini.

Akizungumzia zaidi amesema, uamuzi huu ni kutaka kujiridhisha kutoka kwa watendaji wanaotekeleza maagizo hayo kama wanajua wajibu wao, wanaondoa usumbufu kwa wanachama, na je wanawajali?. Lakini pia kukagua zoezi la kuhakiki wastaafu stahiki zao kabla ya kufanya malipo.

Aidha, amesema atafanya vikao na watendaji hao ili aweze kuwahimiza kujiwekea mikakati ya kuongeza wanachama pamoja na kubana matumizi na namna bora ya kukusanya mapato.

Hata hivyo ametumia fursa hiyo kulipongeza shirika la PSSSF tawi la mkoa wa Singida kwa huduma zake bora kwa wanachama wake na ameliagiza kutenga muda katika kujitangaza zaidi kwa kutumia njia mbalimbali za matangazo, vikiwemo vyombo vya habari vilivyopo ndani ya mkoa, akielekeza zaidi kuitumia redio iliyopo mkoani hapa, STANDARD RADIO ili taarifa ziwafikie haraka wananchi wa mkoa wa Singida.

Wakati huohuo, Mwalimu mstaafu ambaye ni mwananchama wa PSSSF aliyekutwa akipatiwa huduma ndani ya ofisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Bi. Magreth Mfaume, alitumia fulsa hiyo kwa kuzungumza na Mheshimiwa Waziri Jenesta Mhagama huku akianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapatia wananchi wa Tanzania Rais Dkt. John Magufuli anayejali wananchi wote bila ubaguzi wa aina yoyote na kuahidi kumuombea Rais na familia yake kwa ujumla ili wazee waendelee kufurahia heshima ya ustaafu wao.
  
"Huyu Rais tuliyenaye ni zawadi kutoka kwa Mungu, uamuzi wa Desemba mwaka jana, sisi wastaafu tumeupokea kwa mikono yote. Uamuzi wake huo nina uhakika utatuongezea siku za kuendelea kuishi hapa duniani. Kwa sasa baada ya maagizo hayo tunaishi kwa amani kubwa mioyoni mwetu” Amesema mstaafu huyo, Bi. Magreth Mfaume.

Hata hivyo, baadhi ya Wastaafu wengine ambao wameanza kupata huduma mbalimbali katika mfuko wa PSSSF wameonyesha kufurahishwa na huduma wanayopewa na kuishukuru Serikali kwa kurejesha kikokotoo cha asilimia 50.

Kabla ya kuanza ziara hiyo Waziri MHAGAMA alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa mkoa wa SINGIDA Dkt. REHEMA NCHIMBI pamoja na Watendaji wengine na kuhimiza ushirikiano katika utendaji wa kazi.

MATUKIO KATIKA PICHA
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi (kushoto) akisalimiana na Mheshimiwa  Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. JENISTA MHAGAMA, mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wakwanza kulia),  kwa ziara ya kikazi ya siku moja, kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ili kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu. 

 Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili (kushoto) akisalimiana na Mheshimiwa  Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. JENISTA MHAGAMA, mara baada ya kuwasili mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku moja, kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ili kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu.

 Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Victoria Ludovick  (kushoto) akisalimiana na Mheshimiwa  Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. JENISTA MHAGAMA, mara baada ya kuwasili mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku moja, kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ili kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu.

 Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bw. Wilson Shimo (kushoto) akisalimiana na Mheshimiwa  Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. JENISTA MHAGAMA, mara baada ya kuwasili mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku moja, kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ili kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu.






 Watendaji wengine wa Taasisi mbalimbali mkoa za Singida (kushoto) wakisalimiana na Mheshimiwa  Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. JENISTA MHAGAMA, mara baada ya kuwasili mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku moja, kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ili kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu.

 Mheshimiwa Waziri, JENISTA MHAGAMA akipokea taarifa fupi ya Mkoa na kuzungumza na Watendaji wa Taasisi mbalimbali za mkoa wa Singida kabla ya kuanza ziara kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF ili kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu. 


 Mheshimiwa Waziri, JENISTA MHAGAMA akisisitiza jambo kwa Watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF mkoani Singida. 

 Watendaji wa Taasisi mbalimbali za mkoa wa Singida wakisikiliza kwa makini maagizo yaliyokuwa yakitolewa na Mheshimiwa Waziri, JENISTA MHAGAMA (hayupo pichani) kwa Watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF mkoani Singida, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. JOHN MAGUFULI kuhusu kikokotoo cha Mafao ya kustaafu


 Mheshimiwa  Waziri. JENISTA MHAGAMA, akiwasikiliza baadhi ya  baadhi ya Wastaafu ambao wameanza kupata huduma mbalimbali katika mfuko wa PSSSF tawi la Singida.


 Huduma zikiendelea
.



  
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA

No comments:

Post a Comment