Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akisalimiana na Viongozi
mbalimbali wa Wilaya ya Singida DC mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Kilimo Mazao,
kilimo cha umwagiliaji na mfumo wa masoko wa mazao ya wakulima kupitia
ushirika, mkoani Singida.
Naibu Waziri
wa Kilimo Omary Mgumba akikagua bonde la Ntambuko lililopo kijiji cha Kinyeto
wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Singida.
Naibu Waziri
wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza na wakulima (hawapo pichani) wanaotekeleza kilimo
cha umwagiliaji kwenye bonde la Kinyeto Ntambuko Singida vijijini.
Muonekano wa bwawa la
Msange lililopo Singida vijijini.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini
Elia Digha (kushoto) akimuonesha Naibu Waziri mradi wa skimu ya umwagiliaji
unaotekelezwa kwa tija kubwa ya wakulima wa kata ya Msange mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Kilimo
Omary Mgumba akikagua shamba la vitunguu vinavyolimwa kupitia teknolojia ya
umwagiliaji kwa njia ya matone katika kijiji cha Msange mkoani Singida.
Mkurugenzi wa kiwanda cha kukamua alizeti cha
Simai, Juma Mene (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba
alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mtinko Singida DC.
Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini Justine
Monko akizungumza na wananchi wa AMCOS ya Ughandi wanaojishughulisha na kilimo
cha pamba muda mfupi kabla ya kumkaribisha Naibu waziri wa Kilimo.
Naibu Waziri wa Kilimo
Omary Mgumba akizungumza na wananchi wa AMCOS ya Ughandi wanaojishughulisha na
kilimo cha pamba halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini wakati wa ziara
yake.
Meneja wa Uhusiano na
Utumishi wa kiwanda cha Mount Meru Singida Bw. Nelson Mwakabuta akisoma taarifa
fupi ya kiwanda hicho mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba muda mfupi
baada ya kutembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake mkoani Singida.
Mkurugenzi wa kiwanda
cha Singida Fresh Oil Mill, maarufu Kilimo Kwanza, Khalid Ally Omary akimuonesha Naibu Waziri wa Kilimo
Omary Mgumba (katikati) aina ya mbegu mbalimbali za alizeti zinazofaa kwa
uzalishaji bora wa mafuta ya kupikia. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini,
aliyemwakilisha mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima.
Mkutano ukiendelea
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akiangalia
sehemu ya uzalishaji unaofanywa na kiwacha cha kukamua alizeti cha Singida
Fresh Oil Mill, maarufu Kilimo Kwanza wakati wa ziara yake.
Mkurugenzi wa kiwanda
cha kukamua mafuta ya alizeti cha Choice Kindai, Bi. Amina Dang’ati akimuonesha
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba sehemu ya uzalishaji unaofanywa na kiwanda
hicho, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Mgumba mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Kilimo
Omary Mgumba (watatu kutoka kushoto waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja
na wafanyakazi na uongozi wa kiwanda hicho. (kushoto waliosimama ni Mbunge wa
Singida Kaskazini Justine Monko).
Kwa habari zaidi tembelea: http://www.singida.go.tz
No comments:
Post a Comment