Tuesday, December 13, 2016

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA KIKUBWA CHA KUTENGENEZA MAFUTA YA ALIZETI MKOANI SINGIDA.Mkurugenzi Mtendaji (Group Excutive Director) kampuni ya Mount Meru Millers, Atul Mittal (kushoto) akimwonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim mitambo ya kuchuja mafuta ya alizeti kwa kiwango cha kimataifa iliyopo kwenye kiwanda cha mjini Singida. Mhe Majaliwa alifanya ziara kwenye kiwanda hicho na kuagiza viwanda vya ndani viongeze kuzalishaji zaidi wa bidhaa zao ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza nje ya nchi.


Mkurugenzi Mtendaji (Group Excutive Director) kampuni ya Mount Meru Millers, Atul Mittal (kushoto) akimwonyesha Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mafuta ya alizeti yaliyochujwa  kwa kiwango cha kimataifa tayari kuuza ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji (Group Excutive Director) kampuni ya Mount Meru Millers, Atul Mittal (kushoto) akimwonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mashudu ya alizeti yanayonunuliwa na kampuni ya Mount Meru tawi la Singida na kusangwa upya na kutoa mafuta ya kutosha.Mkurugenzi Mtendaji (Group Excutive Director) kampuni ya Mount Meru Millers, Atul Mittal (kushoto) akimwonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mafuta safi ya alizeti ambayo yamechujwa na kuwa na sifa ya kuuzwa ndani na nje ya nchi.Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akipanda mti wa kumbukumbu ya yeye kufanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha Mount Meru Millers tawi la Singida mjini.

Picha na Gasper Andrew.

No comments:

Post a Comment