Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim akizungunza kwenye kilele cha
Baraza la Maulid taifa lililofanyika katika kijiji cha Shelui wilaya ya Iramba
Mkoani Singida. Majaliwa amewahakikishia waumini wa madhehebu ya dini
mbalimbali kuondoa wasi wasi juu ya matukio ya ugaidi kwakuwa serikali iko
macho katika kupambana na tishio lolote la kiusalama ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania.
Sheikh Mkuu na Mufti
wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ally akitoa nasaha zake kwenye kilele
cha Baraza la Maulid taifa lililofanyika katika kijiji cha Shelui wilaya ya
Iramba Mkoani Singida. Pamoja na mambo mengine Mufti amewataka waumini wa dini
ya kiislamu na Watanzania wote kuelekeza nguvu zao katika kufanya shughuli
zitakazowaingizia kipato.
Baadhi ya waumini wa
wilaya ya Iramba na Mkoa wa Singida kwa ujumla waliohudhuria Baraza la Maulid
taifa lililofanyika katika kijiji cha Shelui wilaya ya Iramba.
Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa, amepongeza BAKWATA kwa
hatua yake ya kuanzisha kituo cha DAARUL MAARIF (nyumba ya maarifa ) kwa ajili
ya vijana wa kiislamu kufundishwa elimu ya dini ya ile ya kawaida, ili
kuwafanya wawe waislamu bora na raia wema nchini.
Waziri
mkuu ametoa pongezi hizo, juzi wakati akizungumza kwenye kilele cha Baraza la
Maulid yaliyofanyika kitaifa katika kijiji cha Shelui, wilaya ya Iramba mkoani
Singida.
“Ni
matumaini yangu kuwa chombo hicho ambacho mnapanga kukianzisha nchi nzima,
kiendeshwe kitaalamu na kwa ualedi wa hali ya juu. Lengo ni kiwe endelevu na
pia kifundishe stadi za kazi ambazo zitawasaidia vijana wa kiislamu kujikwamua
kutoka kundi la umaskini”,alisema.
Aidha,
aliangiza chombo hicho kitumiwe vizuri kuaanda vijana wawe makini na wenye
maono na busara ya kuwa viongozi bora kwenye taasisi ya BAKWATA na
taifa kwa ujumla.
“Fanyeni
chombo hicho kiwe chem Chem ya fikra za kuleta maendeleo, kutetea haki na
kupambana na maadui wa taifa hili yaani umaskini , ujinga, maradhi
na ufisadi”, amesisitiza.
Alisema
hana shaka chini ya uongozi wa Mufti Sheikh Abubakar, chombo hicho pia
kitaifanya BAKWATA itoe mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii nzima ya
Watanznia kama yanavyofanya mashirika na taasisi za dini zingine hapa
nchini.
Pamoja
na pongezi hizo alisema amefarijika sana na maboresho kadhaa yanayoendelea
ndani ya BAKWATA ikiwemo uhakiki wa mali ya Baraza.
Awali
Sheikh mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zeberi bin Ally, alitumia
fursa hiyo kuhimiza mshikamano miongoni mwa waumini wa madhehebu
mbali mbali ya dini, ili Tanzania iendelee kubaki kisiwa cha amani
na utulivu.
Aidha,
amewataka waumini wa kiislamu na wasio waislamu kufanya kazi halali kwa bidii
ikiwemo biashara, kilimo na ufugaji ili kujikomboa kiuchumi.
Katika
hatua nyingine, Mufti alisema katika kipindi hiki nyumba nyingi hazina
darasa la malezi kwa vijana kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,kitendo
kinachochochea maadili kuporomoka kwa kasi kubwa.
“Majumba
yetu sasa ni matupa hayana darasa la malezi mema. Hatua hiyo imetupeleka pabaya
maadili na heshima imeporomoka. Zamani mtoto akimwona mtu aliyemzidi umri
alikuwa anamkimbilia na kumsaidia kubeba mzigo hadi nyumbani kwa mtu huyo. Sasa
hivi tabia hiyo njema , imetoweka”,amesisitiza.
Akifafanua
Mufti Ally, alisema kijana wa sasa anajiona hana sababu ya kumpokea mzigo
mtu aliyemzidi umri, mzee/mtu aliyemzidi umri kijana umri,naye amejawa na hofu
kubwa kwamba akimkabidhi kijana mzigo wake mzigo huo, hautakuwa
salama”,alisema.
Kwa hali
hiyo, alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi/walezi kujenga utamaduni wa kutoa
malezi bora kwa watoto wao,ili kulijenga taifa lenye watu wanaomwogopa Mungu waadilifu,
waaminifu na wazalendo kwa nchi yao.
Picha/taarifa na Gasper Andrew.
No comments:
Post a Comment