Thursday, May 02, 2019

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAFANYAKA (MEI MOSI, 2019) ZILIVYOFANA MKOANI SINGIDA



 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kulia) akiongoza shamrashamra za mapokezi ya Wafanyakazi ili kusherehekea kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida.














Wafanyakazi wakiwasili uwanjani ili kusheherekea kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida.


 Wafanyakazi wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa MSHIKAMANO katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Namfua katika Manispaa ya Singida mkoani Singida.

  Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Mbalamwezi cha Manispaa ya Singida kikitoa burudani katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Namfua katika Manispaa ya Singida mkoani Singida.

 Katibu wa TUGHE mkoa wa Singida akisoma risala kwa mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Namfua katika Manispaa ya Singida mkoani Singida.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mgeni rasmi), Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (MB) pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakiongoza shamrashamra za Mei Mosi 2019 kimkoa iliyofanyika katika uwanja wa Namfua katika Manispaa ya Singida mkoani Singida. 

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (MB) akizungumza na wafanyakazi wakati wa sherehe za mei mosi 2019, zililofanyika katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida.

Aidha, Mhe. Sima akizungumza na wafanyakazi hao pamoja na wananchi waliojitokokeza katika maadhimisho hayo ya mei mosi 2019, amesisitiza juu ya kupiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mifuko hiyo.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mgeni rasmi) akizungumza na wafanyakazi wakati wa sherehe za Mei Mosi 2019, zililofanyika katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Dkt. Nchimbi amewapongeza wafanyakazi wa mkoa wa Singida kwa moyo wao wa kazi na utendaji mzuri kwa huduma bora kwa wananchi na kuwataka wafanyakazi wote kumtanguliza Mungu katika utumishi wao ili kulinda maslahi na rasilimali za nchi  ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa Tanzania.

"Tunaposema Singida yetu ni njema tena ni njema sana, tunatambua na kusherehekea matunda ya kazi za mikono yenu" Dkt. Nchimbi.

Aidha, amewapongeza wafanyakazi wa ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kuunga mkono kauli yake ya 'MSHAHARA WANGU UKO WAPI?' kuonyesha mishahara yao katika kilimo, ufugaji wa kuku, viwanja vya makazi, ujenzi n.k.

Hata hivyo Dkt. Nchimbi ametoa onyo kali kwa taasisi za kifedha ambazo hazijasajiliwa kisheria, ambazo hutoa mikopo isiyo rafiki kwa wafanyakazi mkoani Singida kutoka mara moja ndani ya mkoa na kuwataka wafanyakazi hao kuacha kwenda kwenye taasisi hizo na badala yake kutumia taasisi za kibenki zinazotambulika kisheria nchini.

"Na leo ninatoa onyo, waheshimiwa wakuu wa wilaya, kuna watu na vikundi vinakopesha wafanyakazi, wamechukuwa hata ATM na password, wanakopesha wafanyakazi katika halmashauri za wilaya, wafanyakazi wanakuwa watumwa, hizo taasisi.... MWISHO WENU LEO". 

Pia Dkt. Nchimbi amewasisitiza wafanyakazi ambao wamepatiwa zawadi na hati za mfanyakazi bora 2019 kutumia vizuri tuzo na zawadi walizotunukiwa ili kuonyesha thamani ya mfanyakazi bora.

Katika kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, la mikoa yenye madini kuanzisha soko ndani ya siku 7 alizotoa, Dkt. Nchimbi amesema, mkoa wa Singida tayari umetekeleza.

"Tuna soko la dhahabu na soko hilo lipo katika jengo linalotumiwa na ofisi ya madini mkoa, hapo ndipo palipo na soko la dhahabu, na hivi leo ununuzi na uuzaji unaanza. Lakini pia tutakuwa na vituo vitakavyotumika kwa ajili ya kukusanyia dhahabu ndani ya mkoa" 

"Ni ninyi wafanyakazi ndio mnaowezesha Serikali kufanya mambo makubwa ya maendeleo nchini". amesema Dkt. Nchimbi. 

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mgeni rasmi) akikabidhi zawadi ya fedha  na hati ya mfanyakazi bora kwa Bw. Issa Ahmady ambaye ni mhasibu ofisi ya mkuu wa mkoa Singida, wakati wa sherehe za Mei Mosi 2019, zililofanyika katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mgeni rasmi) akikabidhi zawadi ya fedha  na hati ya mfanyakazi bora kwa Bw. Frank John Lawi ambaye ni mchumi katika idara ya Serikali za mitaa katika ofisi ya mkuu wa mkoa Singida, wakati wa sherehe za Mei Mosi 2019, zililofanyika katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida. 

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mgeni rasmi) akimpongeza na kukabidhi zawadi ya fedha  na hati ya mfanyakazi bora kwa Afisa Muuguzi Bi. Christowelu Barnabas ambaye pia ni mratibu wa afya, mama na mtoto mkoa wa Singida, wakati wa sherehe za Mei Mosi 2019, zililofanyika katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida. 

Wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za mkoa wa Singida wakishuhudia makabidhiano ya zawadi na hati kwa wafanyakazi bora, wakati wa sherehe za Mei Mosi 2019, zililofanyika katika uwanja wa Namfua, Manispaa ya Singida mkoani Singida.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA

No comments:

Post a Comment