Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, amewaagiza
wahandisi katika halmashauri zote mkoani Singida kuwa karibu wakati
wote katika kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya ujenzi ndani ya halmashauri
zao yakiwemo majengo ya Serikali pamoja na makazi ya wananchi ili
kuepukana na majanga yanayoweza kusababisha maafa.
Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, sambamba na kukabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau, taasisi na mashirika mbalimbali nchini kwa wananchi hao ambao hivi karibuni nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Amesema, lengo kuu ni wawe na uwezo wa kutoa ushauri, elimu na maelekezo
kwa mafundi pamoja na wananchi ili waweze kujenga majengo yatakayohimili
majanga.
Uzoefu unaonyesha kwamba nyumba au majengo mengi yanajengwa
chini ya kiwango kutokana na wahusika kutokuwa na elimu yoyote ya
ujenzi bora. Majengo ya aina hiyo upepo mkali ukitokea ni lazima
zianguke au mabati yaezuliwe.
Jengo
la soko la kuuzia samaki
“Kwa vile tunao wahandisi wachache, hawawezi kuzungukia majengo
yote yanayojengwa kwenye halmashauri husika, hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa watendaji wa vijiji na kata wapewe mafunzo ya awali kuhusu ujenzi wa majengo
bora na imara, wasimamie na kuhakikisha majengo yanakuwa ya viwango vinavyostahili”, Amesema
Dkt. Nchimbi.
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel
Luhahula, amewataka wananchi wa kijiji cha Doromoni kushiriki kikamilifu kwa
kusaidia mchanga, maji na shughuli zingine muhimu katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa na zahanati zilizokumbwa na upepo huo mkali hata kusababisha uharibifu
katika majengo hayo.
Pia mkuu huyo wa wilaya, ametumia fursa hiyo kumpongeza mbunge
wa jimbo la Iramba Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kutoa msaada wa mifuko 150 ya
saruji, na Katibu Mkuu wizara ya maji, Profesa Kitila Mkumbo mifuko 100 ya
saruji.
Aidha, Amemshukuru meneja wa shirika la World Vision kanda ya
kati Bw. Faraja Kulanga, kwa msaada wa mabati ya aina mbalimbali 773 yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18.1.
Naye, meneja wa shirika la World Vision kanda ya kati Bw. Faraja
Kulanga amesema, kati ya mabati yaliyotolewa na shirika hilo; 208 (geji 28) ni
kwa ajili ya vyumba vitatu shule ya msingi Doromoni, 96 kwa ajili ya jengo la
zahanati ya kijiji, 469 (geji 30) kwa ajili ya Kanisa, jiko la soko na kaya 39.
"Tunaendelea kuhimiza jamii kuchukua tahadhari mbalimbali mapema juu ya
kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea". amesema Bw. Kulanga.
Wakati huo huo, wahanga wa janga hilo lililotokea aprili 9, mwaka huu, wameipongeza na kuishukuru Serikali ya halmashauri ya wilaya ya
Iramba kwa misaada yao ya hali na mali walioitoa wakati wote wa maafa hayo.
Aidha, wamezishukuru taasisi na mashirika mbalimbali likiwemo Shirika la World Vision na wadau
wengine kwa misaada yao ambayo itawafanya kujenga majengo yenye ubora na imara
ili huduma zilizokuwa zikitolewa hapo awali ziendelee kutolewa kwa wananchi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Doromoni wilayani Iramba wakitoa shukrani zao kwa Serikali na wadau mbalimbali waliojitokeza katika kutoa misaada.
MATUKIO MENGINE KATIKA PICHA
Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Emmanueli Luhahula, akizungumza na wananchi wakati wa kikao cha makabidhiano ya misaada mbalimbali iliyotolewa kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Meneja wa shirika la World Vision kanda ya kati Bw. Faraja Kulanga, akizungumza na wananchi wakati wa kikao cha makabidhiano ya misaada mbalimbali iliyotolewa kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza wakati wa kikao cha makabidhiano ya misaada mbalimbali iliyotolewa kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akipokea mabati kutoka kwa Meneja wa shirika la World Vision kanda ya kati Bw. Faraja Kulanga kwa ajili ya kuezeka majengo ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Emmanueli Luhahula, akimshukuru Meneja wa shirika la World Vision kanda ya kati Bw. Faraja Kulanga kwa msaada wa mabati ya kuezeka majengo ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akikabidhi mabati kwa mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Emmanueli Luhahula, yaliyotolewa na shirika la World Vision kanda ya kati kwa ajili ya kuezeka majengo ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akisisitiza jambo kwa mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Emmanueli Luhahula, juu ya mabati yaliyotolewa na shirika la World Vision kanda ya kati kwa ajili ya kuezeka majengo ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Emmanueli Luhahula, akisisitiza jambo kwa mheshimiwa Diwani wa kata ya Turia Bw. Wilfred Jackson Kizaga, juu ya misaada mbalimba iliyotolewa na taasisi na mashirika mbalimbali kwa ajili ya majengo ya wakazi wa kijiji cha Doromoni katika halmashauri ya wilaya ya Iramba ambao baadhi yao nyumba zao zilidondoshwa na zingine kuezuliwa na upepo mkali.
IMETOLWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA
No comments:
Post a Comment