Friday, April 12, 2019

RC SINGIDA ATEMBELEA MIRADI YA KILIMO CHA ALIZETI NA PAMBA, KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA




Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, jana Aprili 11, 2019 amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Mashamba ya Alizeti na Pamba pamoja na ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida, ambapo amewapongeza watendaji wa halmashauri hiyo kwa utendaji wao  na usimamizi mzuri na amewataka kuendelea na kasi hiyo ili kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya Tano.

Dkt. Nchimbi akizungumza na watendaji hao ambao baadhi yao ni waajiriwa wapya amesema, kasi ya utendaji wa awamu ya Tano ni  kubwa sana, hivyo watendaji lazima wabadilike kwa lazima na kuwa chachu ya kubadilisha utendaji na utumishi ili kuendena na kasi ya Serikali iliyopo madarakani.

“Mmeajiriwa ili muwe mbegu mpandwe, muote na mstawi, mbegu ya kuleta mabadiliko ya uhakika ya utendaji wetu ili yaendane na kasi ya awamu ya Tano", 

“Ili utendaji na watendaji tusaidiane kujitambua na kukiri kwamba nyinyi ni watendaji wa Serikali iliyopo madarakani na sio utendaji wa posho, sio utendaji wa mshahara. TIMIZA WAJIBU WAKO”. Kwa msisitizo zaidi amesema Dkt. Nchimbi.

Mkuu huyo wa mkoa amewaagiza maafisa kilimo wote mkoani Singida kutembelea mara kwa mara mashamba ya wakulima sambamba na kuangalia namna bora ya kuwashauri kilimo chenye tija ili kupata mavuno mengi zaidi kwa manufaa ya wakulima katika kuinua uchumi wao, mkoa na taifa kwa ujumla.

Kwaupande wao, Wakulima wa kilimo cha Alizeti katika halmashauri ya Mkalama wamesema, mbegu waliyoipanda msimu huu aina ya HYSUN 33 (Chotara) ni nzuri sana ukilinganisha na mbegu za asili zilizozoeleka kupandwa hapo awali.

Wakulima hao wamesema, aina hii ya mbegu (Hysun 33) hustawi vizuri mashambani hadi kupelekea eka 1 kutoa magunia 18 na mbegu zake zinamafuta mengi ukilinganisha na mbegu za asili hutoa magunia 3 hadi 5.

“Mashamba yangu yamestawi vizuri, hakika mbegu hii ni nzuri tofauti na ile mbegu ya asili tuliyoizoea, kwasababu kwanza aina hii ya mbegu mpya haiweki vichipukizi vya pembeni na inauhakika wa kuzaa hata kama suke limekuwa kubwa". 

"Ile mbegu ya zamani kama suke limekuwa kubwa sana unakuta haina kitu, lakini hii mbegu mpya (Hysun 33) suke lake linakuwa kubwa na linauhakika wa kuwa na kiini. 
Pia inachanua kwa wakati, mfano hapa nimepanda mwanzoni mwa mwezi wa pili”. Amesema George Peter.

Imeelezwa kuwa, Uzalishaji wa mafuta yanayotokana na mbegu ya hysun 33 hutoa asilimia 40 ya ubora wa mafuta wakati mbegu za asili ilikuwa ikitoa asilimia 16.

Naye, mkulima wa zao la Pamba (eka 7), katika kijiji cha Kibii Kata ya Msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida Bw. Joram Samson, ameiomba Serikali kumpatia dawa (sumu) ya kupulizia miche ya zao hilo la pamba ili kukabiliana na changamoto za wadudu wanaoweza kushambulia pamba.

Mkulima wa zao la Pamba (eka 7), katika kijiji cha Kibii Kata ya Msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida Bw. Joram Samson.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, amemuhakikishia mkulima huyo wa pamba kushughulikia changamoto hiyo haraka iwezekanavyo na kuwaagiza maafisa kilimo kuwa karibu na wakulima wakati wote ili kutatua changamoto zao pamoja na kuwaelimisha, kutumia lugha rahisi ili kuleta matokeo mazuri ya mavuno yenye tija.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akikagua kitumba katika shamba la zao la pamba (eka 7) la Bw. Joram Samson, katika kijiji cha Kibii Kata ya Msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Hata hivyo, amewataka wakulima mkoani Singida kutumia muda wao katika kukagua mashamba yao kila wakati ili kufanya shamba kuwa bora na lenye tija kwa mavuno mengi.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akipokea maelezo ya kilimo cha zao la pamba kutoka kwa Afisa kilimo wa hamashauri ya wilaya ya Mkalama Bw. Cuthbert Mwinuka, katika shamba la Bw. Joram Samson, katika kijiji cha Kibii Kata ya Msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akiwa na Afisa kilimo wa hamashauri ya wilaya ya Mkalama Bw. Cuthbert Mwinuka, wakikagua kitumba katika shamba la zao la pamba (eka 7) la Bw. Joram Samson, katika kijiji cha Kibii Kata ya Msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.


Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi. Jackson Masaka akikagua kitumba katika shamba la zao la pamba (eka 7) la Bw. Joram Samson, katika kijiji cha Kibii Kata ya Msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Mkulima wa zao la Pamba (eka 7), katika kijiji cha Kibii Kata ya Msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida Bw. Joram Samson akikagua kitumba.

 Shamba la Bw. George Peter, la zao la Alizeti (Hysun 33) lililopo kijiji cha Nduguti halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka (wa kati) na mkulima wa zao la Alizeti Bw. George Peter  (kushoto), wakati wa ziara yake kukagua miradi ya kilimo cha Alizeti katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkulima wa zao la Alizeti (Hysun 33) katika kijiji cha Nduguti halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida Bw. George Peter akieleza maendeleo ya hali ya zao hilo.


 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa pili kulia), Mkuu wa wilaya ya Mkalama (Wa kwanza kulia), mkulima wa zao la Alizeti Bw. George Peter  (katikati) pamoja na baadhi ya wakulima wakiwa katika picha ya pamoja.

Mkulima wa eka 15 zao la Alizeti (Hysun 33) katika kijiji cha Nduguti halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida Bw. Winfred Msengi akieleza maendeleo ya hali ya zao hilo.


Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisisitiza jambo kwa maafisa kilimo pamoja na wakulima wa zao la Alizeti wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya kilimo cha alizeti na pamba katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kofia) akifuatana na viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Mkalama (Nduguti), wakati wa ziara yake katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.



Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo na Wahandisi wanaosimamia ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Mkalama (Nduguti), wakati wa ziara yake katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

 Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi. Jackson Masaka (kushoto) akizungumza na kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ili azungumze na watendaji wa vijiji, kata pamoja na baadhi ya watumishi waliohudhuria kikao cha kujadili kuhusu tathimini ya zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida. 

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na watendaji wa vijiji, kata pamoja na baadhi ya watumishi waliohudhuria kikao cha kujadili kuhusu tathimini ya zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Watendaji wa vijiji, kata pamoja na baadhi ya watumishi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) wakati akizungumza katika kikao cha kujadili kuhusu tathimini ya zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mkalama.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akizungumza na walimu wa shule za msingi, wawezeshaji ngazi ya wilaya (DITs), wakati wa ziara yake katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto) akizungumza na walimu wa shule za msingi, wawezeshaji ngazi ya wilaya (DITs), wakati wa ziara yake katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Walimu wa shule za msingi, wawezeshaji ngazi ya wilaya (DITs), wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani), wakati wa ziara yake katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, (kulia) akiwa katika moja ya zoezi la mafunzo ya mbinu za kufundisha na kujifunza umahiri wa kuhesabu, alipowatembelea  walimu wa shule za msingi, wawezeshaji ngazi ya wilaya (DITs), wakati wa ziara yake katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi. Jackson Masaka.


Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule za msingi, wawezeshaji ngazi ya wilaya (DITs), wakati wa ziara yake katika hamashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA 
SINGIDA

No comments:

Post a Comment