Saturday, April 27, 2019

MKOA WA SINGIDA WAZINDUA KAMPENI YA WIKI YA CHAJO, IKIWATAKA WAZAZI KUHAKIKISHA BINTI ZAO WANAPATIWA CHANJO HIZO.

MKOA wa Singida umeadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chajo mbalimbali ikiwemo ya polio ili kumkinga mtoto dhidi ya maradhi ambayo yanazuilika kwa chajo.
  
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, amewataka wananchi kuendelea kuuenzi Muungano kwa kuwa umeendelea kudumisha mshikamano na undugu baina ya Watanzania wa bara na wa Zanzibar.

“Sisi sote wakazi wa mkoa wa Singida wajibu wetu ni kuendelea kuuenzi na kuulinda Muungano huu muhimu kwa maendeleo yetu”

“Tuutumie vizuri kwa kuhakikisha tunanufaika na fursa mbalimbali ikiwemo ya uchumi zilizopo ndani ya muungano ili  kujiletea maendeleo katika mikoa na Tanzania kwa ujumla”. Dkt. Nchimbi.

Kuhusu chajo, Dkt. Nchimbi amesema chajo huokoa maisha ya mtoto kwa kumkinga dhidi ya maradhi ambayo yanazuilika.

Amesema, chajo haipo kisiasa..., kupata chajo ni jambo la lazima kwa vile inalinda pia kizazi kijacho dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

“Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya duniani, zimeonesha kwamba chajo ni salama hazina madhara yoyote. Kutokana na ukweli huo, hakuna sababu itakayomzuia mtoto kupata chajo ya aina yoyote”, 

"Huduma za chanjo zimeleta mapinduzi makubwa katika kulinda afya ya jamii pengine kuliko huduma zozote za kitabibu na hivyo kuokoa vifo vya mamilioni ya watu duniani kote" Dkt. Nchimbi.

Akizungumzia chajo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi, Dkt. Nchimbi amewaasa wanafunzi  wa kike waliopata chajo hiyo, kusoma kwa bidii ili waweze kufikia ndoto zao.

Awali, mratibu wa chajo mkoa wa Singida, Bi. Jadil Mhanginonya, amesema kati ya Januari hadi Desemba mwaka jana, jumla ya watoto 66,054 walipata chajo ya kwanza ya Pentavalent. Chajo  ya Pentavalent ni kinga ya kudumu ya magonjwa hatari ya homa ya ini, pepopunda, kifanduro, dondakoo na mafua makali.

Kati ya watoto 66,054 waliopata chajo ya kwanza ya Pentavalent, kati yao ni 61,021, ndio waliomaliza dozi tatu. Watoto 5,033 hawakufika kumalizia dozi ya tatu. Hii ni hatari kwa afya zao. Katika miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu ,pia watoto 18,566 walipata dozi hizo, waliomaliza dozi kamili ni 16,722 wengine 1,844,hawakumalizia dozi.

Mratibu huyo amesema, kwa ujumla katika kipindi cha Januari 2018 hadi Machi mwaka huu, jumla ya watoto 6,877, wameshindwa kumalizia dozi ya chajo hiyo muhimu katika maisha yao.

Wakati huo huo, mkazi wa kijiji cha Ndago, Agweda Nkuwi, amesema dawa pekee ya kumaliza tatizo la baadhi ya watoto kutokumliza chajo ni elimu ya kina kutolewa juu ya madhara  ya kutokukamilisha dozi ya chajo.

Maadhimisho hayo na uzinduzi wa chajo umefanyika katika kijiji cha Ndago katika halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa ndani na nje ya  tarafa ya Ndago.

MATUKIO KATIKA PICHA



 Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akipokelewa na viongozi mbalimbali wa chama, dini na Serikali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maadhimisho ya uzinduzi wa kampeni ya wiki ya chanjo kimkoa yaliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Sehemu ya wanafunzi wa shule za msingi waliojitokeza kushuhudi sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.
  



 Wananchi mbalimbali waliojitokeza kushuhudi sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba akizungumza wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Mratibu wa chajo mkoa wa Singida, Bi. Jadil Mhanginonya akitoa taarifa ya hali ya chanjo kwa mkoa wa Singida wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.
  
 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mheshimiwa Emmanueli Luhahula akizungumza wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kisemeo) akizungumza na kuwapongeza wananchi wenye umri wa miaka 55, wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Wananchi wenye umri wa miaka 55 wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani), wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na viongozi wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wenye umri wa miaka 55, wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

  Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa sambamba na kikundi cha burudani, wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano  ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya  Iramba, mkoani Singida.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA

No comments:

Post a Comment