Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifunua pazia kuashilia ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kusindika mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers Ltd mkoani Singida. Kushoto kwake amemshikilia Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi ishara ya umoja na mshikamano katika Uchumi wa Viwanda.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kusindika mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers Ltd Mkoani Singida. Kutoka kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, Mkurugenzi wa Kiwanda Mount Meru Bw. Atul Mittal, Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ysharose Matembe na kutoka kushoto kwa Mhe. Rais Magufuli ni Waziri wa Viwanda Charles Mwijage, Mfanyakazi wa Mount Meru (aliyeshika sahani), Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba (MB) na Mbunge wa Singida Mhe. Musa Sima wakati wa ufunguzi wa kiwanda.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimpongeza Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kusindika mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers Ltd Mkoani Singida
Mapema mwezi huu, Mhe. Rais Magufuli alitoa pongezi hizo alipotembelea Kiwanda cha kusindika mafuta ya kupikia ya Alizeti cha Mount Meru Millers Ltd kilichopo Mkoani hapa Singida kwa lengo la kukifungua rasmi na kuongea na Wananchi wa Singida na Tanzania kupitia vyombo vya habari.
Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Mkurugenzi
wa Kiwanda cha mafuta cha Mount Meru Millers Ltd Bw. Atul Mittal kwa uamuzi
wake mzuri wa kuwekeza Kiwanda hicho kilichopo katikati mwa Nchi yetu ya Tanzania
na kuwaagiza waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi, Mawaziri na wengine wote kutengeneza
mazingira mazuri ya kuvitunza na kuvilinda Viwanda kama hicho cha Mount Meru
mkoani Singida. “Wewe uliyeamua kuwekeza
kiwanda hapa mkoani Singida tena katikati mwa nchi ni uamuzi mzuri hujakose”
Alisema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemuakikishia Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Mount Meru Millers Ltd kuwa Serikali ya awamu ya tano anayoiongoza itahakikisha
kero zote ndogondogo kuondolewa mapema.
Rais Magufuli alisema, “Kwakweli Singida leo
mmenifurahisha ndio maana nimekuja kwa gari sikutaka kuja kwa ndege ningeishia kuona mawingu tuu, leo nimeona Singida ilivyo pambika, kila mahali pamelimwa mahindi, ulezi, alizeti, Mhe. Mkuu wa Mkoa hongera sana, wakuu wa Wilaya hongera,
Madiwani hongereni Wabunge hongereni Singida mmeibadirisha its looks so nice kila
mahali green, ukigeuka huku mazao huku mazao, Baghosha, hii ndio dhana halisi ya hapa kazi tuu". alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli alimpongeza Mhe. Mbunge
mpya wa jimbo la Singida Magharibi Mhe. Jastine Monko kwa kuchaguliwa kwake na
kuridhishwa na utendaji wake wa kazi kwa kipindi kifupi tu mara baada ya
kuchaguliwa.
Rais Magufuli alisema kuwa nchi yoyote isiyokuwa na Viwanda haiwezi kujenga Uchumi wake
hivyo itaendelea kuwa msindikizaji wa maendeleo. “Tulikuwa na Viwanda
vingi, wakatudanganya kubinafsisha Viwanda vyetu, vingine tukaviuza kwa bei ya
kutupa kumbe lengo lao lilikuwa kuuwa Uchumi wetu. Hakika hiyo haikuwa mbinu ya
kawaida”. Alisisittiza Rais Magufuli.
Alisema kuwa sasa tumeanza kuwa na Viwanda na
kwamba wenye Viwanda vya Mafuta ya kula hapa nchini wanaleta faida nyingi,
ikiwemo Ajira, kulipa Kodi, Umeme na Maji hivyo wanahitaji kulindwa ili waweze
kuhimili ushindani wa wafanyabiashara wanaoleta mafuta hayo kutoka nje.
Alisema, kwa vile hawezi kupiga marufuku uagizaji
huo, njia pekee ya kuwavunja moyo wanaoagiza mafuta kutoka nje ni kuwatoza kodi
kubwa ili waache, na badala yake waanze kujenga Viwanda ndani ya nchi ya Tanzania.
"Kwa sasa nchi inazalisha asilimia 30 tu
ya mafuta ya kula na asilimia 70 kuagiza nje kwa fedha za kigeni hii ni aibu, lazima wafanyabiashara wetu wawekeze ndani ya Nchi yetu Tanzania kwa kujenga Viwanda vingi vya
kutosha, hapo hakutakuwa na sababu ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi wakati wapo
wafanyabiashara wanaoweza kujenga Viwanda humu Tanzania” alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli akiendelea na hotuba yake
iliyogusa hisia za Wananchi waliofika katika viwanja vya uzinduzi huo pia alionya
kwa Wafanyabiashara wenye tabia ya kukwamisha maagizo mbalimbali kwa kurubuni
Wabunge, hivyo alitaka tabia hiyo kuachwa mara moja.
Aidha, Rais Magufuli aliagiza wahusika kuangalia
namna nzuri ya kuwapunguzia kodi wenye Viwanda vilivyopo hapa nchini ikiwa ni
moja ya njia ya kulinda Viwanda hivyo.
Mhe. Rais ametoa mwito kwa wakazi wa Mkoa wa
Singida kulima zao la Alizeti kwa wingi ili liweze kutosheleza mahitaji na Kiwanda
hicho pamoja na vingine huku akimtaka mmiliki wa Kiwanda hicho Bw. Atul Mittal kuwalipa
Wakulima bei nzuri pindi waletapo Alizeti.
Wageni waalikwa wakati wa kushuhudia ufunguzi rasmi wa Kiwanda cha kusindika Mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers Ltd.
Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Singida wakicheza ngoma ya asili ya Kinyaturu kabla ya mgeni rasmi Mhe. Rais Magufuli kuwasili kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika mafuta ya Alizeti.
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Singida wakifurahia jambo wakati wa hutuba ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli alipokuwa anaongea na wananchi. Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula akifuatiwa na Kamanda wa Jeshi la Akiba Mkoa Singida Mussa Simengwa.
Awali Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi
alimshukuru sana Mhe. Rais Magufuli kwa kukubali kuja Mkoani Singida kwa ajili ya
kukifungua Kiwanda hicho ambacho Dkt Nchimbi alikizungumzia kuwa ni Kiwanda
kibubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na Kati.
Dkt. Nchimbi aliongezea kwa
kusema kwamba Mkoani Singida kuna Kiwanda cha kuchenjua dhahabu kinachomilikiwa
na Mwanamke. Naye mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2017 aliyetoka Mkoani Singida mara baada ya kumaliza kazi ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2017 aliweza kuanzisha Kiwanda cha Maziwa.
Akihitimisha hotuba yake fupi, Mhe. Dkt. Nchimbi alimalizia kwa
kusema Hospitali ya Makiungu na St. Gaspar hospital ya rufaa wanazalisha maji ya dripu lakini kwa
kutosheleza mahitaji yao. Alisema kuwa amemuomba Mhashamu Baba Askofu Bernald
Mapunda wa Jimbo Katoliki la Singida kutengeneza Kiwanda kikubwa cha Maji ya dripu kwaajili ya mahitaji yote ya kiafya katika hospitali zote za hapa nchini Tanzania
na nje ya nchi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Wageni waalikwa wakati wa kushuhudia ufunguzi rasmi wa Kiwanda cha kusindika Mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers Ltd.
Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Singida wakicheza ngoma ya asili ya Kinyaturu kabla ya mgeni rasmi Mhe. Rais Magufuli kuwasili kwenye hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika mafuta ya Alizeti.
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Singida wakifurahia jambo wakati wa hutuba ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli alipokuwa anaongea na wananchi. Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula akifuatiwa na Kamanda wa Jeshi la Akiba Mkoa Singida Mussa Simengwa.
“Tunakushukuru sana Mhe. Rais kwa heshima kubwa uliyotupa ya kuja kutufungulia Kiwanda hiki cha kusindika mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Miller Ltd. Hii ni ishara kubwa kwamba Singida ni njema sana, ni bora na inafaa kwa uwekezaji wa Viwanda kwa ukubwa wa aina yoyote” Alishukuru kwa kusema Dkt. Nchimbi.
Mungu Ibariki Singida, Mungu Ibariki Tanzania
No comments:
Post a Comment