WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WILAYANI IRAMBA WACHANGIA MADAWATI 300 KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI.
Mkuu wa Wilaya ya
Iramba Mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula na Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Wakili. Boniface Engelberth Kalikona
wamekabidhiwa madati 300 yenye thamini ya shilingi za Kitanzania
milioni 30 kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo katika Mgodi wa Sekenke Nkonkilangi
Wilaya ya Iramba kwa ajili ya shule za sekondari na misingi wilayani
Iramba ili kuunga mkono jitihada za serikali.
Akizungumza juzi na
wachimbaji wadogo katika machimbo ya Sekenke yaliyopo katika Kijiji cha Nkonkilanga,
Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, Wilayani Iramba alipokuwa katika viwanja
vya mgodi wa Sekenke Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewashukuru sana kwa
ushirikiano wao na kwa kujitoa kuchangia madawati.
Aidha Mkuu wa Wilaya
ya Iramba amewaomba wachimbaji wadogo wadogo kuifadhi na kutunza mazingira ili
yawe mazuri kwa lengo la kuepukana na Magonjwa ya milipuko.
Makundi ya wachimbaji
waliochangia madawati ni Sekenke One Madawati 115, Iramba Nkulu
Madawati 20, Iramba Kenkang’ombe Madawati 135, Mgodi wa Mzizini Madawati
10 na hapa kazi tu Madawati 20.
PICHA ZA MADAWATI YALIYOPOKELEWA NA MKUU WA WILAYA IRAMBA
Madawati yaliyochangiwa na kikundi cha wachimbaji wadogo IRAMBA KENKANG'OMBE mgodi wa Sekenke jumla ya Madawati 135.
Madawati ya kikundi cha wachimbaji wadogo SEKENKE ONE mgodi wa Sekenke jumla ya Madawati 115.
Madawati yaliyochangiwa na kikundi cha wachimbaji wadogo IRAMBA NKULU mgodi wa Sekenke jumla ya Madawati 20.
Madawati yaliyochangiwa na kikundi cha wachimbaji wadogo HAPA KAZI TU mgodi wa Sekenke jumla ya Madawati 20.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba
Mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula (mwenye kofia ya njano waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wachimbaji wadogo wadogo walioungana na kuunda vikundi mbalimbali vinavyojihusisha na shughuli za uchimbaji mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment