Thursday, November 30, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KASSIM MGENI RASMI MAHAFALI YA 33 CHUO KIKUU HURIA, YALIYOFANYIKA MKOANI SINGIDA.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Peter Pinda mara baada ya kuwasili katika mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika leo Mjini Singida, ambapo amekuwa mgeni rasmi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza katika mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika leo Mjini Singida, ambapo amekuwa mgeni rasmi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Peter Pinda.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa (aliyevaa miwani mbele) akiwa na wahitimu wenzake kabla ya kutunukiwa shahada ya Uzamili katika mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Mjini Singida.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Mizengo Peter Pinda akimtunuku shahada ya uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa katika mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Mjini Singida. Wa pili kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifuatiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichaka na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akishuka kutoka katika jukwaa mara bada ya kutunukiwa shahada ya uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera, katika mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Mjini Singida. Pembeni ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Mizengo Peter Pinda  akifuatiw na Wziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akipokea ua kutoka kwa mwanae Saad Majaliwa Kassim mara baada ya kutunukiwa shahada ya uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera, katika mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huri Tanzania yaliyofanyika leo Mjini Singida.


Picha zote kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment