Tuesday, November 28, 2017

MATUKIO YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA BURE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI SINGIDA.

Mmoja kati ya wakazi wa Singida aliyejitokeza kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wenye matatizo mbalimbali wakati wa utoaji wa huduma za afya bure. Huduma za ushauri na matibabu zimetolewa bure kwa muda wa siku mbili za Jumamozi na jumapili kwa ufadhili wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na Chama cha Afya ya Jamii Nchini katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Daktari Misholi akitoa ushauri wa masuala ya Lishe kwa mkazi wa Singida aliyejitokeza kupata huduma za ushauri na matibabu bure ambazo, zimetolewa bure kwa muda wa siku mbili za Jumamozi na jumapili kwa ufadhili wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na Chama cha Afya ya Jamii Nchini katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.

Wananchi waliojitokeza kupata huduma za ushauri na matibabu kwa muda wa siku mbili za Jumamozi na jumapili kwa ufadhili wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na Chama cha Afya ya Jamii Nchini katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Muuguzi wa Masuala ya Lishe Judith Mhoza akitoa ushauri wa masuala ya njia za uzazi wa mpango kwa mwananchi aliyejitokeza kupata huduma za ushauri na matibabu zilizotolewa bure kwa muda wa siku mbili za Jumamozi na jumapili kwa ufadhili wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na Chama cha Afya ya Jamii Nchini katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Mganga Mkuu wa Mkoa Daktari Salumu Manyatta (mwenye koti jeupe) na  Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) Daktari Mashombo Mkamba wakizungumza katika Mkutano wa waandishi wa Habari (hawapo pichani) ili kutoa maelezo ya huduma za matibabu na ushauri zilizotolewa bure pamoja na Mkutano mkuu wa Mwaka wa TPHA.
Baadhi ya wajumbe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) wakisikiliza kwa makini Mkutano wa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakutoa maelezo ya huduma za matibabu na ushauri zilizotolewa bure pamoja na Mkutano mkuu wa Mwaka wa TPHA.
 
YALIYOZUNGUMZWA KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI;
  • Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) kimeanzishwa mwaka 1980, hadi sasa kina wanachama zaidi ya 4000 na matawi 14 nchini kote- Dkt Mkamba.
  • Mkutano Mkuu wa mwaka unaofanyika Mkoani Singida ni wa 34, utafanyika kwa muda wa wa siku tatu ambapo pia kutakuwa na uwasilishwaji wa mada na maandiko ya kisayansi- Dkt Mkamba.
  •  Mkutano huo utafunguliwa rasmi na Naibu Waziri OR-TAMISEMI Joseph Kakunga.
  • Kutokana na kuwa mkutano huo umekuwa wa kisayansi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na chama cha afya ya jamii kiliamua kuandaa huduma bure za afya kwa muda wa siku mbili kama sehemu ya mchango wao kwa jamii- Dkt Manyatta.
  • Huduma za Ushauri na matibabu zilizotolewa ni pamoja na Afya ya Uzazi, Afya ya mama na Mtoto, Huduma za magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari na shinikizo la damu, magonjwa ya macho, Magonjwa yanayoambukiza kama vile VVU na TB, Elimu ya ukatili wa kijinsia, elimu ya usafi wa mazingira na uchangiaji wa damu kwa hiari- Dkt Manyatta.
  • Kwa upande wa Usafi wa Mazingira, Mkoa wa Singida una kaya zenye vyoo kwa asilimia 96 ya kaya laki mbili na elfu tisini, huku asilimia 47 ya kaya zikiwa na vyoo bora na asilimia 4 sawa na kaya elfu kumi na moja zikiwa hazina kabisa vyoo. Inakadiriwa kuwa mtu mmoja huzalisha kilo tisini za kinyesi kwa mwaka- Dkt Manyatta.
  • Kutokana na kuwa Mkoa wa Singida kuwa katikati mwa Tanzania na jirani ya makao makuu ya Nchi Dodoma, kumekuwa na uhitaji mkubwa wa Damu salama, damu inayokusanywa kutoka kwa wale wanaojitolea inapelekwa Tabora kwa ajili vipimo zaidi ili iweze kuwaokoa wagonjwa hasa akina mama wanaojifungua kwa upasuaji na majeruhi wa ajali mbalimbali- Dkt Manyatta.
  • Ugonjwa wa homa ya ini umeonekana kuathiri wananchi wengi kwa siku za hivi karibuni ijapokuwa hatuna takwimu kamili za hali ya maambuki kwa Mkoa wa Singida, ugonjwa huo pia huambukizwa kwa kujamiiana bila kutumia kinga na mtu aliye na virusi ya ugonjwa wa ini, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida inavyo vipimo vya kubaini ugonjwa huo- Dkt Manyatta.
  • Mkoa wa Singida una daktari bingwa wa macho, hivyo wananchi wanaweza kufika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida ili wapate huduma za kibingwa za magonjwa ya macho. Asilimia 70 ya magonjwa yanayosababisha upofu yanazuilika- Dkt Manyatta.

No comments:

Post a Comment