Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionja asali katika moja ya mabanda ya
maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa
ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama bidhaa za mbogamboga katika
banda la Wilaya ya Kondoa katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika
katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika banda
la Mkoa wa Singida katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika
katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Maonyesho
ya nane nane yanatakiwa kuweka alama chanya na kuwa na sura ya mabadiliko yanayoonekana
kwa macho kwa wakulima na wafugaji wanaoshiriki pamoja na wananchi wanaopata
huduma na bidhaa katika maonyesho hayo.
Mgeni
rasmi katika Ufunguzi wa maadhimisho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Chimbi ametoa rai hiyo mapema jana kwa wakulima,
wafugaji na washiriki wakati akifungua rasmi maonyesho hayo huku akiwataka
washiriki hao kuitumia fursa hiyo kwa manufaa zaidi.
“Ni
vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa washiriki mliojitokeza
katika kuonesha bidhaa zenu mbalimbali na pia kwa wale wote waliofika kwaajili ya
kununua au kupata maelezo ya matumizi ya bidhaa hizo, wapate kitu tofauti
kitakachooneka katika maisha yao”, amesema.
Dkt
Rehema Nchimbi ambaye ametumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza umuhimu wa
kuwekeza katika kilimo na ufugaji wenye tija ili kuendana na falsafa ya serikali
ya awamu ya Tano inayo himiza zaidi Uchumi wa Viwanda.
Aidha
ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani na nje ya Nchi wafike kuwekeza
katika mikoa ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa kila atakayekuwa tayari kuwekeza
katika Mikoa hiyo.
“Nimepita kwenye banda la Jeshi la Magereza na
kuona bidhaa nyingi sana zilizotengenezwa na Ngozi na wamenihakikishia kuwa kiwanda
chao kina uwezo wa kununua ngozi yote inayopatikana katika Mikoa ya Singida na
Dodoma hivyo ni vizuri tutumie hiyo kama fursa” ameongeza Dkt Nchimbi.
Dkt
Nchimbi amesisitiza kuwa Mikoa ya Singida na Dodoma haina ukame na ndio maana hivi
sasa ameanzisha mpango maalum wa kilimo cha umwagiliaji kwakuwa watafiti wamewahakikishia
kuwa mikoa hiyo ina kiwango kikubwa cha maji ardhini huku yakiwa karibu na uso
wa ardhi.
Pia
amewataka wananchi wa Mikoa ya Singida na Dodoma kuacha kabisa kukata miti kwa kisingizio
cha kujikwamua kiuchumi kwasababu kuna njia nyingi sana za kuondokana na hilo badala
ya kuharibu misitu.
“Kule
Singida nimeanzisha kampeni inayojulikana kama ‘ACHIA SHOKA, KAMATA MZINGA’
ambayo inampa mwananchi nafasi ya kuamua
kuacha kukata mti na badala yake anafuga nyuki jambo linalomsaidia kujikwamua kiuchumi
kwa muda mrefu zaidi kwasababu unaweza kuukata mara moja tu lakini mzinga unaweza
kuutundika mara nyingi kadri uwezavyo”.
Dkt.
Nchimbi alimalizia hotuba yake kwa kuwasisitiza maafisa kilimo kupeleka kalenda
za kilimo katika ngazi zote kuanzia ngazi ya kijiji ili iwe rahisi kwa Mkulima kujua
aina ya mazao anayoweza kulima kwa Mwaka husika badala ya kumsubiri Mkulima apate
madhara kwanza ndipo aje apewe elimu ya mazao aliyotakiwa kulima kwa mwaka husika.
Maadhimisho
ya 21 ya Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama NANENANE yamefunguliwa rasmi
tarehe 3 Agost 2017 kwa kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Singida na Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionyeshwa shamba la mahindi lilostawi
vizuri katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja
vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa Mkuu
wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Julius Sang’udi alipotembea banda la
jeshi la magereza kujionea bidhaa wanazotengeza katika maonyesho ya nanenane
kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoka katika banda la Tume ya taifa ya
Umwagiliaji, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu katika maonyesho
ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya
Dodoma.
Picha kwa hisani ya domhabari24.
Picha kwa hisani ya domhabari24.
No comments:
Post a Comment