Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikagua ujenzi wa uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Singida.
Uwanja
wa Namfua uliopo manispaa ya Singida ambao ukarabati wake umefikia hatua ya
kuridhisha umeanza kutoa matumaini kwa wananchi wa Singida ambao wamekuwa
wakifuatilia kwa karibu ukarabati wake.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa
Mkoa wa Singida wamefanya ziara ya kushtukiza kujionea hatua iliyofikiwa katika
ujenzi wa uwanja huo ambao utatumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Mpira
wa Miguu iliyobeba jina la mkoa ‘Singida United’.
Dkt.
Nchimbi amesema anaridhishwa na kasi ya utengenezaji wa uwanja wa Namfua
unaomilikiwa cha chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida huku akiupongeza uongozi
wa CCM mkoa wa hatua ilipofikia uwanja huo kwakukwa ni tegemeo la fursa nyingi
hasa za wajasiriamali wadogo.
“Chama
cha Mapinduzi kimetengeneza fursa na ajira nyingi kwa wajasirimali mkoani Singida
kwa kuukarabati Uwanja huu ili uweze kutumika na timu ya Singida United ambayo
inatupa heshima kubwa wana Singida”, ameongeza Dkt. Nchimbi.
Ameongeza
kuwa wananchi wa Singida wana hamu kubwa ya kuziona timu kubwa zinazocheza ligi
kuu Tanzania bara zikicheza katika uwanja wa Namfua na hivyo kuitumia fursa
hiyo kufanya biashara mbalimbali.
Aidha
Dkt. Nchimbi amesema kuwa uwanja huo utakuwa ni chanzo cha mapato kwa mmiliki
wa uwanja huo ambaye ni CCM Mkoa wa Singida, huku timu zitakazocheza, TFF na
Manispaa ya Singida watapata mgao wao kulingana na taratibu zilizopo.
Kwa
upande wao vijana waliokuwa wakishuhudia ukarabati wa uwanja huo wamesema
wamejiandaa kuuza bidhaa kama jezi na vipeperushi vya timu kubwa huku wakisema
watatoa kipaumbele katika kuuza na kuvaa jezi za timu yao ya Singida United.
Wameongeza
kuwa uwanja huo ni faraja kwa kila mjasirimali mkoani Singida wakitoa mfano kwa
wamiliki wa hoteli, nyumba za kulala wageni, wauzaji wa vinywaji na bidhaa
ambazo zinapatikana mkoani Singida kwa ubora mkubwa ambazo ni asali, mafuta ya
alizeti, kuku wa kienyeji, vitunguu bora na Viazi vitamu watapata wateja wa
kutosha.
Uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida ukiendelea kukarabatiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikagua ujenzi wa uwanja wa
Namfua uliopo Manispaa ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Usalama wa
Taifa Mkoa wa Singida.
No comments:
Post a Comment