Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiteta jambo na Makamu wa Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo mara baada ya kukagua maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameridhishwa na maandalizi ya
maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo kitaifa yatafanyika katika
Hospitali ya St. Gasper halmashauri ya Wilaya ya Itigi tarehe 12 Mei, 2017.
Dkt.
Nchimbi amesema hayo mara baada ya kukagua eneo la maadhimisho hayo pamoja na
kukutana katika kikao kifupi na watendaji wa chama cha wauguzi Tanzania na
watendaji wa hospitali ya St Gasper ambapo maadhimiyo hayo yatafanyika.
Amesema
ana imani na uhakika kwa maadhimisho hayo yatafanyika kwa ufanisi mkubwa
kutokana na maandalizi mazurri yaliyofanyika huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atawakilishwa na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.
Dkt.
Nchimbi amewataka wauguzi kuitumia siku yao kuonyesha jinsi fani ya uuguzi
ilivyokuwa ni fani ya upendo, huruma na kujitoa sadaka katika kuhudumia jamii
hivyo wauguzi hao wajitokeze kwa wingi.
Ameongeza
kuwa wananchi wote wa mkoa wa Singida na wale wa halmashauri ya Itigi
wajitokeze kwa wingi ili waweze kushirki maadhimisho hayo kwa kupata huduma
bure na ushauri juu ya masuala ya afya zao.
Kwa
upande wake Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Singida Bi Theresia Ntui amesema
maadhimisho ya siku ya wauguzi yatatanguliwa na shughuli ya maonyesho ya
shughuli za wauguzi.
Amesema
maonyesho yatafanyika katika viwanja vya hospitali ya St. Gasper kuanzia tarehe
10 mpaka 11 Mei 2017 ambapo kutakuwa na huduma za bure kwa wananchi ambazo
zitahusisha upimaji wa sukari, shinikizo la damu, Virusi vya Ukimwi na mafunzo
kwa vitengo juu ya utengenezaji wa uji wa lishe kwa watoto.
Ameongeza
kuwa wananchi wote hasa wazazi wote kuhudhuria mafunzo hayo ya bure ambapo
wataelekezwa hatua kwa hatua namna ya utengenezaji wa uji bora wa lishe kwa
kutumia vyakula asilia ambapo uji huo utawasaidia watoto pamoja na watu wazima
kuwa na afya njema.
Bi
Theresia Ntui amewasihi wauguzi wote Mkoani Singida na Mikoa ya jirani
kuhudhuria maadhimsiho hayo ambapo wauguzi wote watarudia kiapo chao cha uuguzi
pia kutakuwa na maandamano ambapo
watakuwa na fursa ya kuonyesha maoni yao.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiagana na Makamu wa Rais
wa chama cha Wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo mara baada ya kukagua
maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper
Itigi.
No comments:
Post a Comment