Waziri
Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akiwa anatazama asali
inayozalishwa na kikundi cha wazalishaji nyuki Kisaki, Kulia kwake ni
Mkurugenzi wa kikundi hicho Philemon Kiemi.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akizindua kikundi cha
wazalishaji nyuki cha Kisaki katika manispaa ya Singida.
Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza
Peter Pinda Mkoa wa Singida kwa kuzalisha nusu ya asali yote inayopatikana
nchini Tanzania.
Mheshimiwa
Mizengo Kayanza Peter Pinda ametoa pongezi hizo wakati akifunga mafunzo ya
ufugaji nyuki kibiashara wa kikundi cha wafugaji nyuki wa kijiji cha Kisaki
Manispaa ya Singida ambapo aliwatunuku vijana 23 vyeti vya mafunzo hayo.
Amesema
Singida imekuwa ikizalisha tani elfu 17 kwa mwaka huku uzalishaji kwa nchi
nzima ukiwa ni tani elfu 34 kwa mwaka hivyo basi wananchi watumie fursa ya hiyo
kuzalisha asali bora ili ipate soko la kimataifa.
Mheshimiwa
Pinda amesema asali ina faida kubwa kwakuwa imekuwa ikitumika kama chakulana
pia dawa huku akiongeza kuwa baadhi ya wazalishaji wameweza kutumia nta
kuzalisha mshumaa na gundi ijapokuwa bado si kwa kiwango cha kutoshelesha hata
soko la ndani.
Ameongeza
kuwa kuwa wananchi watumie fursa ya nchi ya Tanzania kuwa na misitu hekta
milioni 35 kufuga nyuki kwa wingi ili misitu hiyo iwezwe kutunzwa huku
ikiwafaidisha kwa kuvuna asali na mazao yake.
Mheshimiwa
Pinda amewaasa vijana waliohitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara
kuhakikisha wanaisambaza elimu waliyoipata kwa wenzao pamoja na wao kuwa
wagujai nyuki wa mfano katika maeneo yao.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Singda Elias Tarimo amesema Manispaa ya Singida ina vikundi
16 vya uufugaji nyuki na wafugaji nyuki wengi wakiwa katika kata za Uhamaka,
Mungumaji, Mtamaa, Mwankonko na Kisaki.
Tarimo
amesema wataendelea kuhamasisha vijana na wakazi wengi kufuga nyuki kisasa na
kusisitiza ufugaji nyuki kibiashara ndio wenye tija na manufaa kwa mfugaji.
Mmoja wa
wahitimu Jacob Edward Mashimba amesema mafunzo ni mazuri na yatawasaidia katika
kutunza mazingira kutokana na jamii imekuwa ikikata miti kwa wingi.
Mashimba
amesema katika jamii anayotoka ya kihadzabe ambayo bado inategemea asali kama
chakula kikuu elimu ya ufugaji nyuki kibiashara itasaidia licha ya upungufu wa baadhi
ya vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akimpongeza Jacob Edward
Mashimba kwa kuhitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kabla ya
kumtunuku cheti cha mafunzo hayo.
Eneo
la kikundi cha wafugaji nyuki kibiashara likiwa na mizinga ya nyuki ya
kutosha katika kijiji cha Kisaki, Manispaa ya Singida.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akipata maelezo ya ukamuaji
na upakiaji wa asali kisasa kutoka kwa Mkurugenzi wa kikundi cha
uzalishaji nyuki Philemon Kiemi.
No comments:
Post a Comment