Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisikiliza kwa maelezo ya tathmini ya athari za mazingira na kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta, wa kwanza kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa Dkt Angelina Lutambi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema
Nchimbi (katikati) akisikiliza kwa maelezo ya tathmini ya athari za mazingira na
kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta, wa kwanza kulia kwake ni Katibu
Tawala Mkoa Dkt Angelina Lutambi na kushoto ni Mtathmini wa mazingira Bi Saada Juma kutoka kampuni ya JSB.
Wananchi
wa Wilaya tatu za Makalama, Iramba na Singida Mkoani Singida ambazo bomba la
mafuta kutoka Uganda hadi Tanga linapita wanapaswa kutoka ushirikiano wa kutosha
katika hatua zote za ujenzi wa bomba hilo ili wanufaike na fursa
zitakazopatikana kwa uwepo wa mradi huo.
Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo katika kikao cha tathmini
ya athari za mazingira na za kijamii katika mradi wa bomba la mafuta ambapo
watathmini watapita maeneo yote ambapo bomba hilo litapita ili kupata maoni yao
ili yaweze kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Dkt.
Nchimbi amesema wananchi wanapaswa kuwajulisha watathmini hao kila kitu kuhusu hali
ya mazingira na kijamii ili mradi huo usiharibu mazingira au upunguze baadhi ya
athari wakati wakujenga bomba hilo.
Ameongeza
kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu fidia kwa maeneo ambapo bomba litapita
kwakuwa watalipwa vizuri fidia zao na hivyo wanapaswa kuruhusu mradi huo upite katika
maeneo yao bila wasiwasi na pia wasianze kuendeleza maeneo ambayo wamesikia
mradi utapita kwa kigezo tu cha kupata fidia kubwa.
Kwa
upande wake Mtathmini wa Mazingira Saada Juma kutoka kampuni ya JSB ambayo
inafanya tahmini hiyo amesema wanatekeleza matakwa ya kisheria katika kufanya
tahmini hiyo na wataifanya kwa kasi kubwa ili ujenzi rasmi wa mradi uwahi
kufanyika.
Saada
amesema mradi huo utakua kambi mbalimbali na kwa mkoa wa Singida kambi itakuwa
katika kata ya Msisi ambapo uwepo wa kambi hiyo utaongeza uchumi wa kata na
wilaya hiyo.
Amesema
vijana wa Singida wajiandae kwa ajili ya kupata ajira mbalimali katika mradi
huo, baadhi ya miundombinu itaboreshwa pamoja na uchumi kukukua kwa kuuza
bidhaa na kutoa huduma kwa watakaokuwa wakiishi katika kambi hiyo.
Tathmini
ya athari za mazingira na za kijamii kwa wilaya za Singida, Mkalama na Iramba ambapo
mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka
Tanga itaana mapema wiki ijayo.
Ramani inayoonyesha maeneo ya wilaya tatuza Mkoa wa Singida ambapo tathmini ya athari za mazingira na
kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga.
Wadau wa sekta mbalimbali zinazohusika na mazingira kutoka mkoa wa Singida wakifuatilia kwa umakini maelezo ya tathmini ya athari za mazingira na jamii kwa ujenzi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga.
No comments:
Post a Comment