Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akitoa chanjo kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Wazazi wanaoshindwa
kuwapeleka watoto kupata huduma za chanjo wanakiuka haki za binadamu hasa haki
ya kuishi na pia wanaenda kinyume na juhudi za serikali za kupambana na
maradhi, umaskini na ujinga.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesea hayo katika hotuba yake iliyosomwa na
Mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo wakati wa uzinduzi wa
wiki ya chanjo uliofanyika mapema leo katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya
Singida.
Dkt. Nchimbi amesema
watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano wanapaswa kupata chanjo zote
ili kuwakinga na magonjwa ya homa ya ini, surua, nimonia, kuhara, kifua kikuu, pepopunda na magonjwa mengine ambayo yanazuilika kwa chanjo na motto akiugua kupona ni nadra.
“Mtoto akiumwa
magonjwa hayo kwa kukosa chanjo kupona ni majaliwa na akipona anaweza kupata
ulemavu wa kudumu, hivyo nawasisitiza msipuuze mzingatie kukamilisha chanjo
zote” amesisita.
Ameongeza kuwa
serikali imekamilisha wajibu wake kwa kuhakikisha chanjo zote zinapatikana na
hivyo umebaki wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha mtoto anapata chanjo
pamoja na kuwaelimisha na kuwafichua wale wasiowapeleka watoto kupata chanjo.
Akisoma taarifa ya
hali ya chanjo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Salum Manyatta amesema Mkoa
wa Singida kwa sasa una chanjo zote zinazohitaji na zinatolewa katika vituo 197
kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni katika wiki hii ya chanjo.
Dkt. Manyatta amesema
kwa mkoa wa Singida wananchi wana uelewa wa chanjo ambapo kila mwaka zaidi ya asilimia
95 hufikiwa na chanjo karibia zote huku changamoto ikiwa ni katika kukamilisha
chanjo ambazo huhitaji dozi zaaidi ya moja.
Ameongeza kuwa baadhi
ya wazazi hujifungulia nje ya vituo vya kutolea huduma za afya mfano majumbani
na hivyo kupelekea watoto kukosa chanjo za awali.
Dkt. Manyatta amesema
katika kukabiliana na changamoto za baadhi ya watoto kukosa chanjo, jitihada
zilizowekwa ni pamoja na kupitia kadi ya mtoto kuona endapo amekamilisha chanjo
kabla hajapewa huduma nyingine za afya.
Jitihada nyingine ni
viongozi wa serikali ngazi za vijiji watapewa orodha ya watoto ambao
hawajakamilisha chanjo kutoka katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wawafuatilie wazazi au walezi wakamilishe chanjo hizo pia kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji wa chanjo na kutoa huduma ya mkoba na
kliniki tembezi ili kuwafikia watoto wanaoishi maeneo ya vijijini sana.
Kauli mbiu ya wiki ya
chanjo mwaka huu ni “Chanjo Humkinga Kila Mtu, Pata Chanjo”.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akifurahi mara baada ya kutoa chanjo kwa mtoto wa
umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida
mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali
ya Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo
Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida
mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
No comments:
Post a Comment