Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo (mwenye kofia
nyeupe) akiongoza wakazi wa Manispaa ya Singida kuadhimisha miaka 53 ya
Muungano kwa kufanya usafi sehemu mbalimbali za mji wa Singida jana. Mwenye gloves
nyekundu ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampembile.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amewaongoza wakazi
wa manispaa ya Singida katika kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar kwa kufanya usafi katika sehemu mbalimbali za mji wa Singida.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi,
Tarimo amesema Watanzania wakiwemo wa wilaya ya Singida wanapaswa kuuenzi
Muungano huu kwa kushiriki kikamilifu maadhimisho yake.
Amesema bila Muungano huu ulioasisiwa na viongozi
wetu hayati mwalimu Nyerere na mzee Abeid Karume, Tanzania ya leo isingekuwepo.
“Maadhimisho haya sasa yameboreshwa kwa maana
yanaweza kufanyika kwa kufanya usafi kama tulivyofanya sisi leo au kwa mazoezi
ya mwili. Niwasihi tu Watanzania wenzangu kuyathamini maadhimisho haya na
kushiriki bila kukosa kila mwaka”, amesema.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo
Lyampembile amesema wananchi wa manispaa hiyo wamejitokeza kwa wingi na
kushiriki vema kuadhimisha siku kuu ya Mungano.
“Ofisi yangu nayo imeshiriki watumishi wote ambao
kwa siku ya leo afya zao ziko vizuri, wamejitokeza na kufanya usafi kama njia
ya kuadhimisha siku kuu ya Muungano”, amesema Bravo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo (mwenye kofia
nyeupe) akiongoza wakazi wa Manispaa ya Singida kuadhimisha miaka 53 ya
Muungano kwa kufanya usafi sehemu mbalimbali za mji wa Singida jana. Mwenye gloves
nyekundu ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampembile.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo (mwenye kofia
nyeupe) akiongoza wakazi wa Manispaa ya Singida kuadhimisha miaka 53 ya
Muungano kwa kufanya usafi sehemu mbalimbali za mji wa Singida jana. Mwenye gloves
nyekundu ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampembile.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo (mwenye
kofia nyeupe) akihimiza Watanzania kujenga utamaduni wa kushiriki maadhimisho
ya Muungano wa Tanzania ili kuuenzi. Mwenye gloves nyekundu ni Mkurugenzi wa
Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampembile.
No comments:
Post a Comment