Sunday, October 19, 2014

MPANGO WA USHIRIKIANO WA KUPUNGUZA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WAZINDULIWA.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akifungua mkutano wa mpango wa ushirikiano wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto Mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone amezindua  mkakati wa 'Tokomeza maambukizi mapya ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto Mkoa wa Singida unaoratibiwa na shirika la TUNAJALI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Dokta Kone amesema akina mama wajawazito 8100 na watoto wachanga 48,412 nchini hupoteza maisha kila mwaka hivyo mpango wa ushirikiano wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto utasaidia kupunguza vifo hivyo.

Ameongeza kuwa wataalamu wamesema kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga inawezekana endapo kila mama mjamzito na  mweza wake watahudhuria kliniki kupata maelekezo.

Dokta Kone amesema ili kupunguza vifo  hivyo TUNAJALI kwa kushirikiana  na wadau wake wameanzisha kampeni iitwayo 'Option B plus' inayolenga kuepusha maambukizi mapya ya VVU kwa watoto ambao hawajazaliwa na wale wanaonyonyeshwa na akina mama wenye maambukizi.

Aidha katika kuzindua mkakati huo Dokta Kone amepokea msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 155 kutoka kwa watu wa Marekani na kushauri vifaa hivyo vitumike kulingana na malengo yaliyokusudiwa.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akipokea maelezo kutoka kwa Dokta Asnath Nako wa TUNAJALI kuhusu vifaa vya msaada wa watu wa Marekani.Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akizindua  mkakati wa 'Tokomeza maambukizi mapya ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto Mkoa wa Singida .


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akihutubia wakati akizindua  mkakati wa 'Tokomeza maambukizi mapya ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto Mkoa wa Singida .

Washiriki waliohudhuria uzinduzi wa  mkakati wa 'Tokomeza maambukizi mapya ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto Mkoa wa Singida .
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akishiriki uzinduzi wa  mkakati wa 'Tokomeza maambukizi mapya ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto Mkoa wa Singida .

No comments:

Post a Comment