Monday, August 18, 2014

RS SINGIDA SACCOS YAPATA VIONGOZI WAPYA.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya RAS Singida Saccos Bw. Samson Ntunga mara baada ya kuchaguliwa na wanachama wa Saccos hiyo.

NB RAS Singida Saccos imefanya uchaguzi wa bodi, kamati ya usimamizi na uwakilishi wa Saccos hiyo kutokana na mabadiliko ya sheria ya Ushirika inayotaka vyama vyote vya ushirika nchini kuvunja bodi zilizokuwepo na kuunda mpya.

RAS Singida Saccos imefanya mkutano wa dharura mwishoni mwa wiki na kuwachagua Mwenyekiti Bw. Samsoni Ntunga, Makamu Mwenyekiti Dismas Kimvule, Wajumbe sita wa Kamati ya Usimamizi ambao ni Athumani Bunto, Victor Mkama, Tiluganilwa Mayunga, Dr Abdalah Bala, Erica Charles na Paul Muyinga. Nafasi ya Uwakilishi wa Saccos katika shughuli mbalimbali imechukuliwa na Martin Fute.


Viongozi wa bodi ya RAS Singida Saccos waliochaguliwa mwishoni mwa wiki wakiwa katika picha ya pamoja.

Wanachama wa RAS Singida Saccos walikisikiliza mkutano ulioitishwa ili kuchagu bodi mpya ya Saccos hiyo mwishoni mwa wiki.Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya RAS Singida Saccos Bw. Samson Ntunga akipongezwa  na wanachama wa Saccos hiyo mara baada ya kuchaguliwa.Wanachama wa RAS Singida Saccos walikisikiliza mkutano ulioitishwa ili kuchagu bodi mpya ya Saccos hiyo mwishoni mwa wiki.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya RAS Singida Saccos Bw. Samson Ntunga akitoa shukrani kwa wajumbe wa Saccos hiyo mara baada ya kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Saccos hiyo.

No comments:

Post a Comment