Monday, August 18, 2014

SEMINA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI NA UONGOZI WA SACCOS YAFANYIKA MKOANI SINGIDA.
Bw. Samson Ntunga akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi  Katibu Tawala wa Wilaya Singida Bw. Bura Gwandu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Singida mara baada ya kuhitimu mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa rasilimali za Saccos.

Semina hiyo ya siku Tano iliandaliwa na Muungano wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCULT) na kuwezeshwa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini Bw. Amani Malya na ilikuwa na washiriki kutoka Mikoa ya Dar es Salaam (washiriki 8), Dodoma (washiriki 3), Ruvuma (washiriki 3), Singida (washiriki 12), Mtwara (washiriki 3), Kilimanjaro (washiriki 2) na Pwani (mshiriki 1).


Mgeni rasmi  Katibu Tawala wa Wilaya Singida Bw. Bura Gwandu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Singida akifunga mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa rasilimali za Saccos.

Mshiriki wa mafunzo Bw. Valentine A.  Ndyambi kutoka bodi ya Saccos ya Tanesco Dar es Salaam akisoma risala kwa Mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Singida Bw. Bura Gwandu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Singida.

Mwenyekiti wa Semina hiyo Bw. Kamwana H. Kamwana  akiwa na Mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Singida Bw. Bura Gwandu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Singida.

Washiriki wa mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa rasilimali za Saccos wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment