Tuesday, June 24, 2014

DAFTRARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUBORESHWA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA YA "BIOMETRIC VOTER REGISTRATION".




Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati), kulia kwake ni Katibu Tawala  Mkoa wa Singida Liana Hassan na Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joseph Mchina wakizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Singida (hawapo pichani).

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia mpya ya "Biometric Voter Registration" itakayohusisha vidole kumi vya mpiga kura, picha na saini.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva ameyasema hayo leo wakati akizungumza na nwaandishi wa habari wa Mkoa wa Singida.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati), kulia kwake ni Katibu Tawala  Mkoa wa Singida Liana Hassan wakizungumza na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Singida (hawapo pichani).

Jaji Lubuva ameongeza kuwa zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura linawahusisha wananchi wote yaani waliokwisha jiandikisha, waliotimiza umri wa miaka 18 na wale watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu 2015.

Ameongeza kuwa kutokana na changamoto za Optical Mark Recognition (OMR) ambazo zilipelekea malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali.

Jaji Lubuva amesema pamoja na matumizi hayo ya teknolojia mpya tume ya Uchaguzi imeongeza idadi ya vituo vya kupigia kura kutoka 24,919 hadi kufikia 40,015 vikiwa vimeelekezwa hadi katika ngazi ya vitongoji, mitaa na vijiji.

Waandishi wa habari Elisante Mkumbo wa ITV radio na Jumbe Ismaily wa Channel Ten, wakimsikiliza kwa umakini Jaji Lubuva.

Baadhi ya waandishi wa habari akimsikiliza kwa umakini Jaji Lubuva

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan ameongeza kuwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yameenea hadi vijiji hivyo wananchi hawatapa shida kubwa katika kutumia teknolojia hiyo. 

Hassan amesema Tume ya Uchaguzi inapaswa kupongezwa kwa hatua hiyo inayolenga kuondoa changamoto za teknolojia iliyokuwa ikitumika katika kuandikisha wapiga kura huku akisisitiza elimu kwa mpiga kura itolewe kwa wananchi wote.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati), Kushoto kwake ni Katibu Tawala  Mkoa wa Singida Liana Hassan na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joseph Mchina wakijadili nje ya chumba cha Mkutano.

No comments:

Post a Comment