Thursday, April 10, 2014

ZIARA YA WAZIRI WA MAJI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE MKOANI SINGIDA


Waziri Maghembe akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Kijiji cha Ng'angoli, Wilaya ya Iramba.

Waziri Maghembe akimtwika ndoo ya maji mkazi wa Ng'anguli kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Kijiji cha Ng'anguli, Wilaya ya Iramba.

Waziri wa Maji Jumanne Maghembe jana amefanya ziara ya siku moja Wilaya ya Iramba Mkoani Singida kuzindua na kutembelea baadhi ya miradi ya maji wilayani humo.

Katika ziara hiyo Waziri Maghembe amezindua mradi wa Maji wa Kijiji cha Ng'anguli na kutembelea Kijiji cha Ulemo na Tarafa ya Kinampanda ambapo miradi ya maji inatarajiwa kujengwa.

Waziri Maghembe amesema Wizara yake itatenga Sh milioni 600 kwa ajili ya Mradi wa Maji Tarafa ya Kinampanda na Sh. milioni 800 kwa ajili ya mradi wa maji kijiji cha Ulemo.

Waziri Maghembe akiwasalimia wananchi na viongozi wa Tarafa ya Kinampanda kabla ya kuwahutubia na kutoa ahadi ya ujenzi wa mradi wa maji katika tarafa hiyo.

Waziri Maghembe akihutubia wananchi wa Ulemo na kutoa ahadi aya ujenzi wa mradi wa Maji katika kijiji hicho.

Waziri amewashauri wanakijiji ambapo miradi hiyo inatekelezwa, kuitunza miradi hiyo pamoja na miundombinu kama ya mabomba ili miradi hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kupanda miti na kutunza mazingira katika maeneo ya mradi ili kutunza vyanzo hivyo pia amewashauri viongozi wa kamati za maji za vijiji kutoa taarifa ya mapato ya uuzaji wa maji hayo na matumizi kila baada ya mwezi. 
 
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya maji ya kijiji cha Ng'anguli Paulo Saida amesema bei ya maji kwa lita 20 ni sh 25 ambapo tangu mradi huo ukamilike mwezi Disema 2013 wameshakusanya mapato ya sh milioni saba.

Saida amesema umewasaidia wanakijiji kupunguza kero ya maji ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.

Mjumbe wa kamati ya maji ya kijiji cha Ng'anguli Paulo Saida, nyuma yake ni Tanki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Ng'anguli.

Wanakijiji cha Ng'anguli wakifurahi pamoja na Naibu Waziri Nchemba baada ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho.

No comments:

Post a Comment