Wednesday, November 30, 2022

Wakurugenzi Watakiwa kukamilisha Ujenzi ifikapo Desemba 15, 2022

Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Singida wametakiwa kukamilisha na kukabidhi vyumba vya madarasa ifikapo tarehe 15 Desemba, 2022

Maelezo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, leo akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Manyoni na Itigi.

Akiwa katika shule ya Sekondari Itigi iliyopo Halmashauri ya Itigi Serukamba alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji kutumia fedha za ndani kuongeza chumba kingine cha darasa katika shule hiyo kwa kuwa ilionekana kuwepo kwa mahitaji zaidi.

Shule zilizotembelewa Wilayani humo ni shule ya Sekondari Itigi, Sanjaranda na Kimadoi huku akiahidi kutembelea kata ya Mitundu siku zijazo kwa ajili ya ukaguzi huo.

RC Serukamba ameagiza viongozi wote wa Halmashauri kutoka ofsini na badala yake watembelee miradi hiyo na kuiandikia taarifa huku akimtaka Mhandisi wa Mkoa Domicianus Kirina, kuhakikisha anatembelea miradi yote ya Wilaya hiyo na kuhakikisha ubora wa kazi pamoja kukamilisha kwa wakati.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametembelea Wilaya ya Manyoni katika shule za Makutopora, Malewa, Salanda na Muhalala.

Hata hivyo amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa hatua nzuri waliyoifikia katika mradi huo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Aidha akiongea baada ya ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, amesema Wilaya ina jumla ya vyumba vya madarasa 95 ambapo 10 yapo Halmashauri ya Itigi wakati vyumba 85 vikiwa katika Wilaya ya Manyoni.

Kwa upande wake Kaimu Afisa elimu wa Mkoa Fredrick Ndahani, amesema fedha zilizokuja kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Wilayani Manyoni ni Bilioni 1.7 na zilizotumika mpaka sasa ni Milioni 640.86

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA ZIARA 








No comments:

Post a Comment