Thursday, October 03, 2024

RC DENDEGO AZIAGIZA HALMASHAURI KUFIKISHA FURSA MIKOPO YA 10% KWA WALENGWA MPAKA VIJIJINI.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego, ameagiza Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 inawafikia walengwa hadi vijijini ikiwa ni pamoja na akina mama, vijana, watu wenye ulemavu, na wazee ili kuimarisha uchumi wa wananchi na kusaidia maendeleo hadi ngazi za vijiji. RC Dendego ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa Programu ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi "IMARISHA UCHUMI NA MAMA SAMIA (IMASA)" iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano RC Social uliyopo Singida Mjini Octoba 3, 2024.

Kwaupande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, amepongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuridhia mikopo ya asilimia 10 kupatiwa makundi ya akinamama, vijana, watu wenye ulemavu na wazee huku akiwataka kutumia fursa za mikopo hiyo kwenda kuanzisha viwanda vidogo vya uzalishaji nishati mbadala akisisitiza kuwa hatua hii itachangia katika kukuza uchumi wa mkoa na kuboresha maisha ya wananchi.

Ameeleza kuwa nishati mbadala ni muhimu katika kuimarisha maendeleo endelevu na kupunguza utegemezi wa nishati ya kawaida.

No comments:

Post a Comment