Sunday, December 01, 2024

"SINGIDA TUJILINDE NA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU NA UKIMWI":DC GONDWE

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Leo hii katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Disemba Mosi,2024 amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego yakiyoadhimishwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida katika chuo Cha uhasibu kampasi ya Singida.

Akizungumza katika maadhimisho hayo,ametoa wito Kwa vijana kupima afya zao ili kuweza kuziishi ndoto zao nyingi huku akiwasisitiza wanandoa kuwa waaminifu ili kuepuka ongezeko la maambukizi huku akisisitiza tohara Kwa wanaume kama njia mojawapo ya kuzuia magonjwa Kwa wanaume

"Wanandoa wawe waaminifu Kwa wenza wao,pia ni vema kuwapenda,kuwajali na kuwahudumia waathirika WA VVU.Pia ni vema vijana wakaacha tamaa za maisha mazuri ili kuepuka vishawishi ambavyo vinasababisha kujiingizia katika vitendo vinavyoweza kupelekea kupata VVU,kuepuka hilo ni vema kuishi katika uhalisia WA maisha Yao na kupambania ndoto zao za baadae".amesema Gondwe.

Dkt.Said Mgeleka ambaye ni Meneja wa Mradi kutoka USAID amesema kwasasa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI zinapatikana Kwa urahisi na Kwa wingi tofauti na miaka ya nyuma ambapo iliwalazimu watu wa makundi maalum pekee kama wamama wajawazito wakati WA kujifungia pekee na wagonjwa wale ambao CD4 zao zilianza kushuka na kusumbuliwa na magonjwa nyemelezi ndio waliokua wakipata dawa hizo kutokana na uchache wa dawa uliosababishwa na ufinyu WA bajeti 

"Kwasasa dawa za ARV zinapatikana katika ngazi zote sio tu katika hospitali za mikoa na Taifa Bali mpaka katika zahanati zote vijijini kwani tangu 2016 juhudi za Serikali na wadau zimewezesha utoaji wa dawa hizo Kwa yeyote yule atakayegundulika na maambukizi bila Kujali wingi wa CD4 au dalili yeyote ya magonjwa nyemelezi"amesema Dkt.Mgeleka

Amesema pia kwasasa huduma za kinga dhidi ya VVU zimeongezwa Kwa kuleta dawa kinga Kwa watu wote walio katika hatari ya kuambukiza au kupata VVU,Pia kwasasa ni rahisi kupima wakati wowote na mahali popote na Kwa usiri kwani vifaa vya kujipima maambukizi vinapatikana kwa wingi na sio katika vituo vya afya pekee kama wakati wa nyuma.

Amini Nyaungo ni mmoja wa vijana ambao wamejitokeza katika maadhimisho haya amesema kuwaa ameitumia siku hii vema Kwa kupima afya yake pia kupata elimu juu ya VVU NA UKIMWI ambayo ataiwasilisha pia Kwa vijana wengine ambao hawana uthubutu katika kupima na kupata elimu ya VVU na UKIMWI.

"Nitaitumia fursa hii Kwa kuwapa vijana wenzangu elimu juu ya VVU,pia ntawaekimiaha kuhusu matumizi ya dawa kinga Kwa lengo la wao kufahamu Nini wafanye pale ambapo wanaona kuwa wapo katika hatari ya kupata VVU na matumizi Sahihi ya ARV Kwa wale ambao wamegundulika kuathirika na ugonjwa huu ila wana hofu ya kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi"alisema Nyaungo.

Maadhimisho hayo yametanguliwa na maandamano mapema asubuhi,ikifuatiwa na huduma ya kupima afya(VVU NA UKIMWI) na mjadala kuhusu UKIMWI na vijana jinsi gani watajilinda na maambukizi au jinsi gani ya kuepuka kuambukiza wengine VVU. 

Kaulimbiu ya maadhimisho haya mwaka huu ni "CHAGUA NJIA SAHIHI TOKOMEZA UKIMWI"




No comments:

Post a Comment