Wananchi Mkoani Singida wametakiwa kuhakikisha wanawapatia watoto wao wenye umri wa miaka chini ya mitano chanjo ya matone dhidi ya Ugonjwa wa Polio itakayotolewa kuanzia tarehe Moja hadi Nne Desemba, 2022.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Afya ya
Msingi ya Mkoa (PHC) Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba amewataka wazazi na jamii
kwa ujumla kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano anapata
chanjo ili kuwa salama na watu wengine.
Aidha RC Serukamba amefafanua kwamba jumla ya watoto ambao
wanatarajia kupata chanjo ni 443,230 ambapo
Iramba ina watoto 65,074 Singida
Dc watoto 690,557 Manyoni 55,825 Manispaa ya Singida 45,722 Ikungi 97,575 Mkalama 58,905 na Itigi
watoto 51,072.
"Tayari vifaa na chanjo vimekwisha wasili katika vituo mbalimbali vya Afya na Zahanati ambapo huduma nyingine zitakuwa zikitolewa kwa njia ya mkoba nyumba kwa nyumba mtoto baada ya mtoto" alisema Serukamba.
Hata hivyo amewataka wakuu wa Wilaya kusimamia zoezi hilo kuhakikisha
chanjo hiyo inatolewa na inawafikia idadi iliyopangwa katika Wilaya.
Amesema chanjo inayotolewa imedhibitishwa kwamba ni salama
hivyo Serikali haitawavuliwa watu wenye nia mbaya ya kuwapotosha wananchi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamati ya Mkoa ya ulizi na
usalama, viongozi wa Dini mbalimbali, Taasisi, muwakilishi kutoka Wizara ya
Afya TAMISEMI na muwakilishi kutoka
Shirika la Afya duniani.
No comments:
Post a Comment