Baadhi
ya akina mama wa kijiji cha Sepuka wakifuatilia semina ya kupinga
ukeketaji kwa mtoto wa kike iliyoandaliwa na shirika la Women Wake Up
(WOWAP).
Wakazi
wa Kijiji cha Sepuka wilayani Singida wameiomba Serikali kwa
kushirikiana na mashirika binafsi yaendelee kutoa elimu kwa jamii juu ya
madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike kwani jamii hiyo bado
inaendelea kukeketa watoto wa kike wakiwa wachanga.
Wakazi
hao wametoa rai hiyo wakichangia mada katika semina iliyoandaliwa na
shirika la Women Wake Up (WOWAP) linaloendesha mradi wa Kutokomeza
ukeketaji kwa njia ya majadiliano ya vikundi kwa ufadhili wa shirika la
Japan la Women Action Against FGM(WAAF JAPAN).
Nasra
Suleimani Afisa ufuatiliaji na tathmini na Samora Mnyawonga kutoka
WOWAP wakizungumza na wakazi wa Sepuka juu ya madhara ya ukeketaji kwa
mtoto wa kike.
Wamesema
ukeketaji bado unafanyika kwa siri sana kwa kushirikiana na ndugu wa
karibu mfano bibi au shangazi huku wanaume wakiwa wamefichwa juu ya
suala hilo.
Wameongeza
kuwa ndugu wenye umri mkubwa kama bibi na shangazi huwashawishi akina
mama kukeketa watoto wachanga kwa kisingizio kuwa kutampunguzia mtoto
uwezekano wa kupata magonjwa ya mara kwa mara.
Baadhi
ya wanaume walioshiriki semina hiyo wamesema kuwa wamepata elimu ya
madhara ya ukeketaji na wako tayari kuwalinda watoto wao na wengine
dhidi ya ukeketaji.
Wameongeza
kuwa ukeketaji bado unaendekezwa na wazee kwakuwa jamii ya sasa
imeshaelimika hivyo nguvu zaidi ielekezwe kwa wazee ambao huwashawishi
akina mama, aidha wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya
madhara ya ukeketaji katika kliniki za ujauzito.
Samora Mnyawonga kutoka WOWAP wakizungumza na wakazi wa Sepuka juu ya madhara ya ukeketaji kwa mtoto wa kike.
Kwa
upande wake mwezeshaji ambaye ni mratibu wa mradi huo Zuhura Karya
amewataka akina mama na wanaume waliopata elimu hiyo wawe mabalozi wa
kupinga ukeketaji kwa mtoto wa kike na ukatili wowote, pia watoe taarifa
katika vyombo vya usalama wapatapo taarifa za ukeketaji.
Karya amewashauri akina mama kuangalia usafi wa mtoto mchanga kwa kuhakikisha nepi za watoto zinakuwa safi, usafi wao na wa chakula cha mtoto ili kuwakinga watoto wachanga dhidi ya magonjwa na sio kuwakeketa.
Mwezeshaji
ambaye ni mratibu wa mradi wa kutokomeza ukeketaji kwa njia ya
majadiliano ya vikundi Zuhura Karya (mwenye miwani) akiwaelimisha wakazi
wa Sepuka juu ya madhara ya ukeketaji.
No comments:
Post a Comment