Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko
Vicent Kone, ameiagiza jamii kuvunja ukimya kwa kuanzisha utamaduni wa
kuwapatia vijana elimu ya afya ya uzazi na ujinsia ili kuwapatia mbinu za
kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha yao.
Dokta Kone ametoa wito huo juzi wakati
akizungumza kwenye hitimisho la utekelezaji mradi wa ushiriki sawa wa wanaume
katika afya ya uzazi na ujinsia (TMEP) Mkoani Singida.
Amesema jamii inalo jukumu la
kuhakikisha inatenga muda wa kuzungumza au kujadiliana mara kwa mara na vijana
kwa lengo la kuwapa mbinu bora zitakazowawezesha kutimiza ndoto za kimaisha
kama vijana.
Katibu Tawala Miundo mbinu Tiluganilwa
Mayunga akizungmza juzi kwenye ufungaji wa hitimisho la mradi wa ushiriki sawa
wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia (TMEP), Mradi huo wa
miaka minne uliohitimishwa juzi na kukabidhiwa kwa Halmashauri za wilaya ya Manyoni,
Singida na manispaa ya Singida. Kushoto ni Meneja wa TMEP, Cuthbert Maendaenda na
kulia ni meneja wa HAPA, David Mnkaje.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Miundo mbinu Tiluganilwa Mayunga, Dokta Kone ameitumia fursa hiyo kuyashukuru mashirika ya Health Actions Promotions Association (HAPA) na Youth Movement For Change (YMC) kwa kutekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Miundo mbinu Tiluganilwa Mayunga, Dokta Kone ameitumia fursa hiyo kuyashukuru mashirika ya Health Actions Promotions Association (HAPA) na Youth Movement For Change (YMC) kwa kutekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa.
"Nimepewa taarifa kwamba hivi sasa
wanaume wengi wamebadilika na kuwa chachu katika masuala ya afya ya uzazi na
ujinsia.Nimeambiwa kuwa kwa sasa wanaume wanawasindikiza wenza wao kliniki, wanajadili
pamoja uzazi wa mpango na wanafanya kazi zote za nyumbani isipokuwa zile za
kibailojia. Kabla ya ujio wa TMEP wanaume wote walikuwa wanawaachia kazi nyingi
wake zao basi", amefafanua.
Meneja wa shirika lisilo la kiserikali
la Health Actions Promotions Association (HAPA) David Mnkaje akitoa taarifa
yake juu ya kumalizika kwa mradi wa ushiriki sawa kwa wanaume katika masuala ya
afya ya uzazi na ujinsia (TMEP) mbele ya wadau waliofanikisha mradi huo wa
miaka mine uliomalizika mwaka jana. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala Miundo mbinu
Tiluganilwa Mayunga na wa kwanza kushoto ni Meneja wa mradi wa TMEP Cuthirbert
Maendaenda.
Kwa upande wake Meneja wa HAPA David
Mnkaje amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne cha mradi huo wamehamasisha
jamii na kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa njia mbalimbali ikiwemo ya
majadiliano na matumizi ya vikaragosi.
"Pamoja na changamoto za hapa na
pale leo wafanyakazi wa HAPA kwa ujumla wetu tunayofuraha kubwa kwa kuwa
tumefikia kwa kiasi kikubwa lengo la mradi. Kwa sababu hakuna awamu ya pili ya
mradi huu tunaangalia uwezekano wa kuanzisha mradi wa aina hii kati ya Mkoa wa
Manyara na Tabora", alisema meneja huyo.
Naye meneja TMEP Makao makuu Cuthrbet
Maendaenda amesema madhumuni kuu la TMEP ni kila mtu katika jamii awe huru
kutumia haki yake ya afya ya uzazi na ujinsia wakati madhumuni mahususi ni
wanaume wawe chachu ya mabadiliko juu ya mtazamo wao dhidi ya wanawake.
Maendaenda ametaja baadhi ya mikakati
ya kuendeleza mradi huo kuwa, ni pamoja na kutoa mafunzo kwa viongozi
mbalimbali na kuwahimiza masuala ya afya ya uzazi na ujinsia yawe ni ajenda ya
kudumu katika mikutano ya WDC, kamati za afya, VEO, WEO, waelimisha rika, wahudumu
wa afya vijijini.
Katibu Tawala Miundo mbinu Tiluganilwa
Mayunga Tiluganilwa Mayunga (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja
na wadau mbalimbali wa mradi wa ushiriki wa wanaume katika masuala ya afya ya
uzazi na ujinsia baada ya wadau hao kukabidhiwa vyeti kwa ushiriki wao katika
kutekeleza mradi huo wa miaka minne. Kulia ni Daktari bingwa wa maradhi ya
wanawake Mkoani Singida Dokta Suleimani Muttani na kulia ni Meneja wa shirika
la HAPA David Mnkeje.
No comments:
Post a Comment