Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dokta Parseko Vicent Kone amekabidhi mashine 24 za kufyatulia matofali
kwa halmashauri sita za Mkoa wa Singida zilizotolewa na shirka la nyumba ya
Taifa (NHC).
Makabidhiano hayo
yamefanyika leo asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na kuhudhuriwa na wakuu wa
wilaya wote, watendaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watendaji kutoka NHC.
Akitoa neno kwa niaba
ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Kyande Mchechu, Mkurugenzi wa NHC Singida
Ladislaus Bamanyisa amesema shirika hilo limetoa mashine za kufyatua matofali
ili kuisaidiana na Serikali katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Bamanyisa ameongeza
kuwa mashine nne zimetolewa kwa kila halmashauri ambapo zitagawiwa kwa kikundi
cha vijana 40 na shilingi laki tano kama mtaji wa kikundi hicho huku
halmashauri zikiombwa kugharimia mafunzo kwa vikundi hivyo.
Aidha Dokta Kone amelishukuru
shirika la Nyumba la Taifa kwa kutoa mashine hizo zitakazo ongeza ajira kwa
vijana wa Mkoa wa Singida huku akiwataka wakuu wa Wilaya aliowakabidhi mashine
hizo kuhakikisha vikundi hivyo vya vijana vinaundwa na vinakuwa vikundi vya kudumu.
Amewaagiza kila Mkuu
wa Wilaya afuatilie maendeleo ya vikundi hivyo na kutoa taarifa NHC kila baada
ya miezi mitatu ili kuonyesha namna ambavyo msaada walioutoa unaleta tija kwa
jamii.
Dokta Kone amewaagiza
pia wakuu wa wilaya kutenga maeneo kwa ajili ya NHC ili wajenge nyumba bora za
kuwauzia wananchi Mkoani Singida na kusisitiza kuwa mashine zilizotolewa zitasaidia
utekelezaji wa kampeni ya Mkoa ya ‘Ondoa tembe jenga nyumba bora’.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akimkabidhi mashine ya kufyatua matofali Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwl. Queen M. Mlozi.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akizungumza wakati wa makabidhiano ya mashine 24 za kufyatulia matofali kwa Wakuu wa Wilaya.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone na Watendaji wa NHC, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wakuu wa Wilaya.
No comments:
Post a Comment