Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, akizungumza kwenye kilele
cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi Mkoa wa Singida yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa askofu Mabulla mjini Singida. Wa kwanza kulia ni Kaimu meneja wa TRA
Mkoa wa Singida, Samwel Shula na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Queen
Mlozi.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa
wa Singida, imekusanya zaidi ya shilingi 4.14 bilioni kuanzia julai mwaka jana
hadi sasa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 34 ikilinganishwa na shilingi
bilioni 3.09 zilizokusanywa kwa kipindi hicho katika mwaka wa fedha uliopita.
Aidha,wigo wa kodi umeongezeka kwa
kuandikisha walipa kodi kutoka 5,821 mkwa 2012/2013 hadi kufikia walipakodi
6,859 kwa mwaka 2013/2014.
Hayo yamesemwa na kaimu meneja TRA mkoa
wa Singida, Samwel Shula wakati akitoa taarifa yake kwenye kilele cha
maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa askofu Mabula mjini Singida.
Kaimu meneja wa TRA Mkoa wa Singida, Samwel Shula, akitoa taarifa
kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi Mkoa wa Singida. Maadhimisho
hayo yamefanyika kwenye stand ya askofu Mabula mjini Singida. Wa pili kulia
(waliokaa) Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dokta Parseko Kone, anayefuata ni Mkuu wa Wilaya
ya Singida Queen Mlozi na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Liana Hassan.
“Napenda kutambua mchango mkubwa wa
walipa kodi wote na wadau mbalimbali katika eneo hili la kulipa kodi na kwenda
sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu;”Risiti ni haki yako,asiyetoa anakwepa
kodi”, alisema.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dokta Parseko Kone, alisema kumekuwa na
ongezeko kubwa la ukusanyaji wa mapato kuliko ili ya ukuaji wa uchumi katika
kipindi chote ambacho TRA imekuwa msimamizi wa jukumu hili la kukusanya mapato
ya serikali kuu.
“Nawapongeza viongozi na watumishi wote
wa TRA na wadau wote kwa mafanikio haya.Ninatambua kuwa mafaniko haya ni
matokeo ya juhudi na nguvu za watu wengi,wote nawapongeza sana”,alisema
Dokta Kone.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dokta Parseko Kone, (katikati) akimkabidhi cheti cha mdau
wa TRA Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Liana Hassan. Wa kwanza kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Singida. Queen Mlozi na kulia ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa
Singida, Samwel Shula.
Aidha ameiasa TRA mkoani hapa kuongeza juhudi za kukusanya mapato
zaidi na wakati huo huo wahimize utaratibu wa kulipa kodi kwa hiari na
kuanzisha mifumo rahisi na rafiki kwa mlipa kodi. Hii ni pamoja na matumizi
sahihi ya mashine za kieletroniki za kutolea risiti (EFD).
Baadhi
ya wafanyabiashara na wadau wa TRA Mkoa wa Singida, waliohudhuria kilele cha
maadhimisho ya siku ya mlipa kodi yaliyofanyika kwenye stand ya askofu Mabula
mjini Singida.
(Picha/taarifa
na Nathaniel Limu-dewjiblog).
No comments:
Post a Comment