Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone amepokea ugeni kutoka Benki ya Dunia ambao unafanya tathmini ya manufaa ya ujenzi wa mradi wa barabara ya lami ya Singida-Shelui yenye urefu wa kilomita 109.
Akiongoza
ugeni huo jana asubuhi, Afisa mawasiliano kutoka Benki ya Dunia Loy Nabeta amesema lengo ni
kutathmini manufaa ya barabara hiyo iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya Benki
ya Dunia na Serikali ya Tanzania.
Nabeta
amesema licha ya kuwatembelea wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara
hiyo, ugeni huo utazungumza na wasafirishaji ili kufahamu manufaa
waliyoyapata kutokana na ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa
upande wake Dk Kone amesema barabara hiyo ina manufaa makubwa kwa wananchi wa
Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.
Ameongeza
kuwa baadhi ya manufaa hayo ni pamoja na kuongezeka kwa viwanda vidogovidogo
vya kusindika mazao, Ujenzi wa nyumba bora kutokana na upatikanaji wa vifaa kwa
urahisi, ulinzi na usalama kuboreka zaidi kutokana na kufikika kwa uharaka
zaidi katika maeneo mbalimbali.
Dk
Kone amesema katika kuhakikisha barabara zinatunzwa, wakuu wa wilaya, maafisa
Tarafa, watendaji wa kata na wananchi waishio pembezoni wana wajibu wa
kuhakikisha barabara hizo zinatunzwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Dunia,
Wa kwanza kushoto kwake ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida mhandisi Yustaki
Kangole na anayefuatia ni Afisa Mawasiliano toka Benki ya Dunia Loy Nabeta.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akisisita jambo wakati akizungumza na ugeni
kutoka Benki ya Dunia, Wa kwanza kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida
Liana Hassan.
No comments:
Post a Comment