Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt. Parseko V. Kone ametembelewa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini
Tanzania Mhe. Dkt Lu Youqing jana asubuhi ofisini kwake.
Balozi Youqing amefanya ziara mkoani Singida ili kujadili
mipango ya sasa na ya baadaye ya kimaendeleo Mkoani Singida ili kuona maeneo ya
uwekezaji ambayo yatainua pato la mwananchi.
Katika ziara hiyo
Balozi Youqing ameambatana na Mwakilishi Mkuu wa Uwakilishi wa Kiuchumi na Kibiashara
wa Jamhuri ya Watu wa China Nchini Bw. Lin Zhiyong pamoja na Afisa wa Ubalozi
huo Bw. Ren Zhihong.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Parseko V. Kone (katikati) akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini
Tanzania Mhe. Dkt Lu Youqing (wa kwanza kushoto), anayefuata ni Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, wa kwanza kulia ni Mwakilishi Mkuu wa
Uwakilishi wa Kiuchumi na Kibiashara wa Jamhuri ya Watu wa China Nchini Bw. Lin
Zhiyong akifuatiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan, Nyuma yake ni
Katibu wa Mkuu wa Mkoa Hussein Mwatawala.
Amesema wawekezaji
kutoka China wako tayari kuwekeza Mkoani Singinda na tayari kampuni moja kutoka
China imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza katika umeme wa kutumia nishati ya upepo.
Balozi Youqing ameongeza kuwa Tanzania ina hitaji umeme wa
uhakika na wenye gharama ambazo wananchi watazimudu, akisisitizia umeme wa
upepo ambao amesema hauchafui mazingira.
Ameongeza kuwa
wawekezaji kutoka China wanaweza kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji Mkoani
Singida ili kukuza uchumi wa mwana Singida.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Parseko V. Kone akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini
Tanzania Mhe. Dkt Lu Youqing (wa kwanza kulia), anayefuata ni Mwakilishi Mkuu wa
Uwakilishi wa Kiuchumi na Kibiashara wa Jamhuri ya Watu wa China Nchini Bw. Lin
Zhiyong.
Balozi Youqing amesisitiza kuwa kutokana na historia ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China, kwa sasa Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa zina fursa ya kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mikoa nchini China ili kujifunza teknolojia mbalimbali, kutafuta kampuni za uwekezaji na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Ameongeza kuwa ameona
jitihada za dhati zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa katika kuleta maendeleo kupitia
kilimo na ufugaji Mkoani Singida.
Kwa upande wake Dkt.
Kone amemshukuru Balozi Youqing kwa kuonyesha nia ya kushirikiana naye katika
kuleta maendeleo ya Mkoa wa Singida hasa katika kusaidia kupata wawekezaji
katika mradi wa umeme wa nishati ya upepo.
Dkt. Kone amesema mradi
wa umeme wa upepo hautaunufaisha Mkoa wa Singida peke yake bali taifa kwa
ujumla kwa kutoa fursa za ajira, ongezeko la viwanda na umeme wa uhakika.
Ameongeza kuwa
wawekezaji kutoka China wana fursa mbalimbali za uwekezaji Mkoani Singida kama
vile kilimo na ufugaji, akitilia mkazo uwekezaji katika mazao ya alizeti,
vitunguu, pamba na mpunga.
Dkt. Kone amesema
wananchi wa Singida wanafuga Kuku bora wa asili ambapo uwekezaji ukifanyika
utawaongezea kipato.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Mhe. Dkt Lu Youqing (wa kwanza kulia), anayefuata ni Mwakilishi Mkuu wa Uwakilishi wa Kiuchumi na Kibiashara wa Jamhuri ya Watu wa China Nchini Bw. Lin Zhiyong.

Aidha Mkoa wa Singida
unatoa asali bora nchini hivyo uwekezaji katika sekta ya ufugaji nyuki na kiwanda cha
kuchakata asali na nta utaongeza thamani ya mazao hiyo.
Balozi Youqing amekuwa
balozi wa kwanza kuutembelea Mkoa wa Singida kwa Mwaka 2014. Mkoa wa Singida
umewahi kutembelewa na Mabalozi kutoka Ireland, Marekani, Kenya, Nigeria na
Uingereza.
No comments:
Post a Comment