Mwenyekiti wa RS Singida Sacoss Ltd Bw. Samson Ntunga akiwa ofisini kwake.
Mkutano Mkuu wa tano wa RS Singida Sacoss umefanyika siku ya Jumamaosi katika ukumbi wa Mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa, huku ukianisha faida na changamoto za saccoss hiyo.
Mkutano Mkuu wa tano wa RS Singida Sacoss umefanyika siku ya Jumamaosi katika ukumbi wa Mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa, huku ukianisha faida na changamoto za saccoss hiyo.
Akisoma risala kwa Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Sacoss hiyo Samsoni Ntunga amesema tangu kuanzishwa kwake, sacoss hiyo imezidi kuimarika kutokana na ushirikiano mzuri kati ya wajumbe wa bodi na watendaji wa chama.
Mwenyekiti wa RS Singida Sacoss Ltd Bw. Samson Ntunga (katikati) akiwa na wajumbe wa bodi ya sacoss hiyo.
Ntunga amesema moja ya mafanikio ni wanachama kuongezeka kutoka 144 mwaka 2008 hadi kufikia 222 mwaka huu pamoja na kutoa mikopo mikubwa na midogo kwa wanachama yenye thamani ya shilingi milioni 329.
Ameongeza kuwa chama kimebuni mradi wa Viwanja eneo la Mamise Kata ya Mandewa kwa ajili ya wanachama kwa gharama nafuu ambapo mchakato utakamilika mapema April na viwanja hivyo vitakiingizia chama faida ya shilingi milioni 55.
Wanachama wa RS Singida Sacoss Ltd wakiwa katika mkutano mkuu wa tano wa Sacoss.
Wanachama wa RS Singida Sacoss Ltd wakiwa katika mkutano mkuu wa tano wa Sacoss.
Ntunga amesema katika kukabiliana na changamoto ya mtaji mdogo usiokidhi mahitaji ya wanachama ambapo baadhi ya wanachama walikuwa wakikosa mikopo, Chama kimenunua hisa katika Benki ya Ushirika Tanzania.
Ameongeza kuwa wanachama walikuwa wakitaka kukopa kinyume na sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya mwaka 2003 hivyo katika kukabiliana na changamoto hii bodi imeamua kufuata sheria hiyo katika kutoa mikopo.
Wanachama wa RS Singida Sacoss Ltd wakiwa katika mkutano mkuu wa tano wa Sacoss.
No comments:
Post a Comment