Habari za hivi punde
zinasema kuwa, John Tupa, Mkuu wa Mkoa wa Mara, (pichani) amefariki ghafla muda
mchache uliopita.
Kwa mujibu wa mtoa
habari ni kuwa marehemu Tupa, alikuwa akitoka katika moja ya kikao cha utendaji
mkoani kwake ambapo baada ya kupewa Maelezo mafupi alikuwa akielekea eneo
husika kwa ajili ya kutembelea na kukagua kile alichoelezwa katika taarifa hiyo,
na wakati akipanda gari ndipo alipoanguka na kupoteza maisha.
Mungu ametoa na Mungu ametwa, Mungu ailaze
roho ya Marehemu Tupa mahala pema pepon, Amina.
No comments:
Post a Comment