Sunday, April 07, 2024

RC DENDEGO AELEZA KISHINDO CHA MAFANIKIO YA MIAKA 3 YA SERIKALI YA AWAMU YA 6 MKOANI SINGIDA

Mkoani wa Singida leo umejivunia mafanikio lukuki ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Halima Dendego, ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu hiyo kwa kubainisha kukua kwa pato la mkoa na la mwananchi mmoja mmoja.

Dendego ameyasema hayo Aprili 7, 2024 wakati wa hafla fupi ya kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Mkoa wa Singida hafla iliyoambatana na futari kwa baadhi ya viongozi wa Dini, Chama, Wabunge wa Mkoa huo, wadau wa maendeleo pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria.

Akizungumza na viongozi, wadau wa maendeleo na wananchi katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Makazi ya Mkuu wa Mkoa huo mjini Singida, amesema wastani wa pato la Mkoa limeongezeka kutoka Sh.Trilioni 2.709 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Sh.Trilioni 3.196.

Dendego amesema kwa upande wa wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja kwa Mkoa wa Singida umefikia Sh. 1,589,073 mwaka 2022/23.

Aidha, amesema wastani wa ukusanyaji mapato kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni Sh. bilioni 12.382 kwa mwaka na wastani wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa Halmashauri ni Sh.bilioni 16.285.

Dendego amesema katika kipindi hicho Mkoa umepokea Sh. Trilion 1.7 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya uendeshaji shughuli mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, ameeleza kuwa katika kuwainua wananchi kiuchumi, jumla ya Sh. 3,068,836,418 zimetolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye uelemavu na Sh. 2,258,086,426.61 zimetengwa kwa ajili ya kuvikopesha vikundi hivyo mara Serikali itapotoa mwongozo mpya.

Akiendelea na wasilisho lake, Mkuu wa Mkoa huyo amesema Serikali kupitia Mpango wa Kuhudumia Kaya Maskini (TASAF) imerudisha matumaini na furaha kwa takribani kaya 58,090.

Amesema walengwa wameguswa kwa kupatiwa fedha za moja kwa moja kiasi cha Sh. Bilioni 22.083  kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka mitatu Mkoa umepata Sh.12,369,200,000 kwa ajili ya sekta ya kilimo na mifugo. Kutokana na hali hiyo mkoa umeendelea kuwa na usalama wa chakula na wastani wa uzalishaji kufikita tani 984,649.8 kwa mwaka naumepokea tani 1,075.5 za mbegu ya ruzuku ya alizeti yenye thamani ya shs. 5,622,144,000.

Aidha, uzalishaji wa alizeti umeongezeka kutoka tani 145,915.4  kwa mwaka 2020/2021 hadi kufikia tani 482,559 kwa msimu wa 2022/23 na tani 10,151.4 za mbolea ya ruzuku zimetumika zenye thamani ya Sh. 8,396,208,300.

Uanzishaji wa mashamba ya pamoja ya Korosho (Block famrs) umefikia ekari 28,000 toka ekari 25,000 mwaka 20202/21 na wastani wa mavuno kufikia tani 155.7, ujenzi wa skimu 12 na ukarabati wa skimu 3 za umwagiliaji kwa thamani ya Sh. Bilioni 49.7.

Kipindi hicho pia kumejengwa majosho 34, usambazaji wa dawa za mifugo na  pikipiki 197 zilivyogharimu Sh. bilioni 1.411.


Katika sekta ya elimu, Mkoa umepewa Sh.71,105,590,806.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akielezea kwa upande wa sekta ya Elimu amesema, Shule mpya 17 za Sekondari na 12 za Msingi na madarasa 1,469  ya awali, Msingi na Sekondari yamejengwa, majengo ya utawala 12 na nyumba za walimu 65 yamejengwa, maabara 85, matundu ya vyoo 2,194 yamejengwa, mabweni 48 na  mabwalo 6.

Kuhusu vifaa vya kufundishia na kujifunzia vimesambazwa,jumla ya walimu 826 wa msingi na walimu 427 wa sekondari wameajiriwa na uandikishaji na hali ya ufaulu kwa madarasa yote yanayopimwa umeendelea kuimarika.

Hata hivyo, Serikali ya Mkoa wa Singida ilipokea Sh.41,278,488,055 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ambapo hospitali 4 za hadhi ya Wilaya na ukarabati mkubwa wa Hospitali kongwe 3 zimejengwa.

Kazi nyingine zilizotekelezwa ni ujenzi wa vituo vya afya 21 na ukamilishaji wa Zahanati 60, ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za dharura 4 na ICU 3, nyumba za watumishi 6 (3 in 1) na majengo 3 ya huduma za dharura.

Ameongeza kwamba ujenzi wa mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya oxygen na ukarabati wa majengo mbalimbali ya kutolea huduma, kuajiri watumishi 634, kutoa mafunzo kwa watumishi 193 na ununuzi wa vifaa tiba zikiwemo CT Scan na Digital Xrays na kuimarika kwa utoaji huduma za kibingwa na upatikanaji wa dawa.

Katika kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi inaongezeka, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imepewa Sh. 3,962,434,442.37 na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa kipindi hicho imepewa Sh. 19,023,793,102.13.

Uzalishaji wa maji safi umeongezeka kutoka lita za ujazo 8,500.00 kwa siku hadi lita  11,467,000, mtandao wa usambazaji umeongezeka kutoka km 341,45 hadi km 401.10.

Aidha, upatikanaji wa maji umeongezeka kutoka 65% hadi 85% mjini na 57, 9 hadi 67.7% vijijini na utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa mabwawa 5 ya maji taka unaendelea.

Akielezea miundombinu amesema, kiasi cha zaidi ya Sh.bilioni 1 zimeelekezwa kwenye ujenzi wa barabara, madaraja, uwekaji wa taa za barabarani, upembuzi yakinifu kwa miradi mipya ya barabara, ufunguzi wa barabara mpya, ujenzi wa vivuko na makalavati.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, akisoma taarifa ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Mheshimiwa Dendego akizungumzia sekta ya Ardhi amesema, jumla ya Sh. 2,000,000,000 zimetolewa katika Wilaya ya Manyoni DC na Itigi  kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi.

Katika utekelezaji wa mradi huo, jumla ya wananchi 7,049 wakiwemo Wahzabe 150 wamepatiwa hati milki za ardhi zao na vipande vya ardhi 6,439 vimepimwa na makazi 2000 yamepimwa na kurasimishwa. 

Aidha, jumla ya wananchi 1,276 waliopitiwa na bomba la mafuta wamelipwa fidia na wananchi 27 wamejengewa nyumba za kisasa kwa gharama ya Sh. bilioni 2 na katika mradi wa SGR  Lot 5 wananchi 1,411 wametambuliwa hatua za kufikia ulipaji wa fidia zainaendelea.

Kwaupande wa Sekta ya Umeme amesema kuwa, jumla ya vijiji 420 kati ya 441 sawa 95.24% vimeunganishiwa na umeme wa gridi ya taifa toka vijiji 252 mwaka 2020/21 za na ongezeko la vijiji 158.

Wateja 89,623 (wakubwa 51, kati 51,775 na wadogo 37,797) wameunganishiwa umeme na matumizi ya umeme mkoani yameongezeka kutoka 13.92MW (2020/21) hadi 19.86MW (2023/24).

Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, akitoa salamu za Serikali wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Mkoa huo amesema, kuongezeka kwa mapato yatokanayo na uchimbaji wa madini toka Sh. 4.76 bilioni mwaka 2020/21 hadi shs. bilioni 13.7 mwaka 2022/23.

Aidha, vikundi 10 vya wachimbaji wadogo vimepatiwa leseni na kwa mtu mmoja mmoja zimetolewa leseni moja moja 821 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo na ajira 1000 zimepatikana.

Kufunguliwa kwa Mgodi wa Shanta ulioleta faida kubwa kwa mkoa na Taifa kwa kuongeza ajira, mapato, huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo kilimo, maji, elimu na nyinginezo.

Kuongezeka kwa viwanda kutoka 1, 576 mwaka 2020/21 hadi 1,805 ambapo Mkoa kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzanzia (TIC) kubaini, kutenga na kutangaza maeneo yenye ukubwa wa hekta 6,261 kwa ajili ya uwekezaji.

 MATUKIO KATIKA PICHA

Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata, akitoa salamu za chama kwa washiriki wa hafla hiyo.

Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, akitoa salamu za Serikali wakati wa hafla hiyo.


Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akizungumza wakati wa hafla hiyo.





Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, akisalimiana na baadhi ya viongozi mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo iliyofanyika katika makazi ya Mkuu wa Mkoa huyo.



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida akikabidhi zawadi ya mafuta ya alizeti kwa moja ya kiongozi wa Dini ya Kiislamu.




Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga akitoa salamu za shukrani kwa wadau na viongozi walioshiriki kwa hali na mali katika kufanikisha hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment