Tuesday, March 05, 2024

RC SERUKAMBA AKIFUTILIA MBALI KIKUNDI CHA NKIRI KILICHOTUMIKA KAMA POLISI JAMII WILAYANI MKALAMA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, amepiga marufuku shughuli zote za Ulinzi zinazofanywa na jeshi la asili linalojukikana kwa jina la NKILI, Wilayani Mkalama, na kuwataka Wananchi wa Kijiji cha Yulansoni, Kata ya Kinyangiri, wajifunze kwa makosa na waheshimu Sheria za nchi, Ili kudumisha amani na usalama, katika maeneo yao.

Serukamba amesema hayo, alipofika kwenye kijiji hicho, pamoja na mambo mengine kutatua migogoro wa mgongano wa kiutawala, baina ya Serikali ya Kijiji na jeshi la asili la NKILI, lililojichukulia madaraka tangu mwaka 1986, na kuwatoa adhabu kali kwa watuhumiwa, wanaojihusisha na uhalifu, kwenye eneo hilo.

Miongoni mwa.adhabu zinazotolewa na jeshi hilo, ni pamoja na mtuhumiwa kitozwa faini ya fedha, kutengwa na hata kutotakiwa kwenda kwa yeyote, kama njia mojawapo ya kumshikiaha adabu, kwa lengo la kudhibiti uhalifu katika eneo husika.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kwa mkuu huyo wa mkoa kufanikiaha agizo lake, kutokana na upinzania mkàli alioupata kutoka kwa wananchi waliohidhuria mkutano wa hadhara, baada ya kugawangika huku wengine wakiunga mkono na wengine kugomea uwepo wa jeshi hilo la NKILI.

Baada ya kubaini hali hiyo, Serukamba ilibidi atumie njia ya kupiga kura za siri, kupitia karatasi zilizoandaliwa, kwa wale wana

oliunga jeshi hilo kupiga kura ya NDIYO na wanaokataa, kura ya HAPANA, na hapo ndipo wanaopiga wakaibuka washindi kwa kura 110, wanaoafiki kura 28 na kura 22 ziliharibika. 

"Nashukuru leo hii ninyi wenyewe mmeamua kuwa hamtaki kuendelea na NKILI... Mwenyekiti na Serikali yako ya Kijiji hembu njooni hapa, jipange hapa na wajumbe wako Ili wananchi hawa wawaone...," alisema Serukamba.

Baada ya wajumbe wa Serikali ya Kijiji kujioanga msitari, Serukamba aliwataka wananchi kudikisha malalamiko yao ofisini, badala ya jeshi la jadi, Ili matatizo yao yawezd kushughulikiwa kulingana na taratibu za Serikali.

Serukamba aliwaeleza wananchi hao kuwa, Tanzania inaongozwa kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu, hivyo jukumu lote la ulinzi lipo chini ya Serikali yenye vyombo vya ulinzi likiwemo jeshi la polisi na mahakama, na si chombo kingine chochote kile, chenye nia mbaya ya kujipatia kipato.

"Leo ninyi wenyewe hapa mmeamua kuwa hamtaki kusimamiwa na NKILI, mnataka Serikali yenu ya Kijiji mlioichagua iendeshe mambo yenu, kwa hilo mmefanya uamuzi mzuri...,"alibainisha Serukamba.

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI KATIKA PICHA



Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akizungumza na wananchi wakati wa mkutano huo.


Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali, akizungumza wakati wa mkutano huo.

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea.

Kura zikihesabiwa 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akiendesha zoezi la ukusanyaji wa kura zilizopigwa na wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya Wilaya Mkalama akizungumza wakati wa mkutano huo.

burudani zikiendelea mara baada ya mgogoro kutatuliwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali, akishangilia kwa kumalizika kwa mgogoro huo.

Sehemu ya Meza kuu

No comments:

Post a Comment