Akizungumza wakati wa
mafunzo hayo Mratibu msaidizi, Program ya shule Bora, kutoka Taasisi ya elimu
nchini (TET), Mwesiga Kabigumila amesema Wilaya hiyo inanufaika na mafunzo hayo
baada ya utafiti na uchanganuzi wa matokeo ya elimu ya msingi mwaka 2022 kuonyesha
kiwango cha ufaulu somo la hilo kipo chini ya asilimia 34 ikiwa ni cha chini
zaidi kuliko halmashauri zingine sita za mkoa huo.
Kabigumila, alisema mafunzo
hayo yanawahusu walimu wa shule za msingi 50 wa somo la hisabati, waratibu kata
10, walimu wakuu 20 na viongozi wengine mbalimbali, wa halmashauri hiyo na mkoa
wa Singida.
Kwa mujibu wa Mwesiga,
mafunzo hayo yana lengo la kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji bora,
hasa kwenye mahiri zenye changamoto darasani, kwa walimu wanaofundisha hisabati
ili kuleta mageuzi chanya kwa wanafunzi kufanya vyema zaidi.
“Kufanya vibaya kwa
Iramba kwenye elimu ya msingi mwaka 2022, kwa kiwango cha chini sana ya
asilimia 34, imekuwa ni moja ya sababu ya kuleta mafunzo haya, ili walimu
wapate mbinu, zitakazowasaidia katika ufundishaji wa somo la
hisabati,”alifafanua Mwesiga.
Aidha Mwesiga, aliwataka
washiriki kuyaelewe mazingira ya wanafunzi wao wanaowafundisha sambamba na kutengeneza
zana zinazotoka kwenye maeneo yao rafiki kwa ajili ya kuboresha na kusaidia mbinu
za ufundishaji na ujifunzaji somo la hisabati.
Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Singida, Sarah Mkumbo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Singida, Sarah Mkumbo, aliwataka washiriki wazingatie mafunzo yanayotolewa na wataalamu wa elimu, ili mbinu wanazopewa ziweze kuleta tija katika somo hilo, na hivyo kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa wilaya ya Iramba.
Mkumbo amesema kuwa,
pamoja na kazi nzuri inayofanywa na uthibiti ubora katika kutekeleza majukumu ya
kuwasimamia walimu lakini mafunzo wanayofundishwa yatawajenga kiuwezo na hivyo kuwaongezea
maarifa zaidi ya ufundishaji wa kazi zao za kila siku darasani.
MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MAFUNZO HAYO.
No comments:
Post a Comment