Monday, September 25, 2023

MWENGE WA UHURU WAMURIKA MIRADI YA MAENDELEO SINGIDA DC

MWENGE wa Uhuru 2023 umewezesha kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Akitoa taarifa ya miradi ambayo imezinduliwa tarehe 24 Septemba, 2023 na Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili amesema kuwa hupo mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya shule ya Msingi Ikiwi ambapo amesema kuwa mradi huo hupo Tarafa ya Mtinko kata ya Kijota kijiji cha Ikiwi.


Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mosses Machali (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili wakati wa sherehe za mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023.

Muragili amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa tarehe 30 Mei, 2023 na umekamilika 28 Julai, 2023 na kueleza kuwa mradi huo umetumia kiasi cha sh. Milioni 47.

Aidha ameutaja mradi mwingine kuwa ni mradi wa kuzalisha maji tiba katika Hospitali ya Wamisionari wa St. Charles Borromeus Triet chini ya udhamini wa shirika la St. Luke Foundation ambao unahusika kuandaa wataalamu, kuwezesha upatikanaji wa malighafi na kufuatilia ubora wa uzalishaji maji tiba.

Ameeleza kuwa gharama za mradi huo ni sh. Milioni 144.4 kwa uhisani wa Masisiter wa Upendo wa St.Charles Borromeus Triet.

Aidha katika Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu imetolewa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Ukimwi, Muragili amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Singida ina vituo 40 vinavyotoa huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya UKIMWI.

Kwa kipindi cha Julai mwaka 2022 hadi Julai 2023 jumla ya watu waliopimwa VVU walikuwa 40953 kati yao wanaume ni 15,034 sawa na asilimia 37 na wanawake ni 25919 sawa na asilimia 63 waliogundulika na maambukizi ya VVU ni 230 sawa na asilimia 0.6.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kuulaki kuushangilia pamoja na kupata ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu. 

Sambamba na hilo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim amewataka Watanzania hususani wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuepukana na ngono zembe au kuacha kabisa.

Hata hivyo amewahamasisha kupima afya zao na kujua wanahali gani kiafya na pale wanapogungulika kuwa na VVU waanze kutumia dawa bila kuona aibu au kuwa na woga.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim  akigawa vyandarua kwa akina mama wajawazito ili kupambana dhidi ya ugonjwa wa Malaria wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.







Mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Samia Suluhu yenye urefu wa KM 0.5  iliyojengwa katika mji wa Ilongero Halmashauri ya Wilaya ya Singida ambapo Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 ulitembelea.



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 (kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili wakati wakishiriki zoezi la ufunguzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya Msingi Ikiwi iliyopo kata ya Kijota kijiji cha Ikiwi.

No comments:

Post a Comment