WATUMISHI wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Halmashauri za Wilaya na Manispaa mkoani Singida wametakiwa kutumia mfumo mpya wa ununuzi wa umma ujulikanao NeST ulioanzisha na Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) ambapo mtumishi akifanya manunuzi bila kutumia mfumo huo atakuwa ametenda kosa la jinai.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick, ambaye alimwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, alisema hayo kwenye mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka halmashauri zote za mkoa huu kwa siku tano na kuwaeleza kuwa kutumia mfumo huo ni jambo la lazima kwani ni maelekezo mahsusi ya Serikali.
Ludovick alisema mfumo huu mpya wa manunuzi ni dhahili utaleta uwazi zaidi katika taratibu za manunuzi na utaongeza tija kwenye shughuli za Serikali hasa kwenye fedha ambako sehemu kubwa ipo kwenye manunuzi.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Ununuzi Sekretarieti
ya Mkoa wa Singida, Nkuli Nketo alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo
watumishi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ili waweze kutumia mfumo huo mpya
kuanzia Oktoba Mosi 2023 kwa lengo la kuepuka kufanya manunuzi ya aina yeyote
nje ya mfumo wa NeST ambapo mfumo ulivyojengwa utawawezesha watumishi kufanya
manunuzi ya aina yeyote ndani ya mfumo.
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment