Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba leo ameiagiza Taasisi ya kudhibiti na kupambana na rushwa ((TAKUKURU) Mkoani hapo kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kutokomeza rushwa katika maeneo ya kazi ikiwemo rushwa ya ngono ambayo imeonekana kushamiri sehemu nyingi.
Maagizo hayo ameyatoa leo wakati wa sherehe za wafanyakazi
Mei mosi iliyofanyka ki Mkoa katika uwanja wa Liti uliopo Manispaa ya Singida
ambapo alieleza changamoto ya rushwa inavyoweza kurudisha maendeleo nyuma ya
Mkoa huo.
Aidha Serukamba ametoa muda wa kipindi cha miezi mitatu
Taasisi hiyo imletee taarifa ambavyo wametengeneza mikakati ya kupambana na
aina hizo za rushwa.
Kwa upande wake Mratibu
wa TUCTA Mkoa wa Singida, Maria John Bange ameiomba Serikali kuhakikisha watumishi wanalipwa stahiki zao
za kisheria na mafao ya kustaafu kwa
wakati, jambo ambalo mgeni rasmi RC Serukamba alilitolea maelekezo kwa
Wakurugenzi kuhakikisha wanalipa stahiki hizo huku akitoa maelekezo kwa Shirika
la Bima na NSSF kuhakisha wanawalipa mafao kwa wakati.
Hata hivyo Mratibu huyo ameomba Serikali kuhakikisha mabaraza ya
wafanyakazi yanafanyika kwa wakati na uwepo wa staha katika sehemu za kazi.
No comments:
Post a Comment