Watendaji wa Serikali Mkoani Singida wametakiwa kujifunza na kutumia taaluma ya huduma kwa mteja (costumer care) ili kutoa huduma inayowaridhisha wateja wao na kupunguza kero kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo 28/4/2023 na Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Peter Serukamba wakati alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi wa Manispaa ya
Singida katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi
Stadi (VETA).
Amesema changamoto nyingi zinasababishwa na lugha mbaya za Watendaji
wa Serikali ambao wameamua kutojali maslahi ya wengine hivyo kuwataka kutumia
lugha zenye staha kuwajibu wateja wao na kujiwekea taratibu za kuwapa elimu
kabla ya kufanya maamuzi.
Kero nyingi zilizoletwa na wananchi kwa Mkuu wa Mkoa zilikuwa
ni migogoro ya viwanja, changamoto ya ulipaji wa pensheni kwa wastaafu kupitia
mfuko wa NSSF, migogoro ya familia na
umilikishwaji wa ardhi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt.
Fatma Mganga, Mkuu wa Wilaya ya Singida Muhandisi Paskas Muragili, Mstahiki
Meya, Wahandisi, Kamati ya ulinzi na usalama na maafisa elimu kata pamoja na
wakuu wa Taasisi.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment