Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba leo ameendelea na zoezi la utatuzi wa kero za papo kwa hapo katika Wilaya ya Ikungi kata ya Sepuka Kijiji cha Mnang'ana ambapo kero 52 zilisikilizwa na kupatiwa ufumbuzi .
Akiwa Kijijini hapo RC Serukamba alipokea kero za ukosefu wa maji, Barabara, migogoro ya ardhi na uharibifu wa maziringira ambapo alitoa maagizo kwa menaja wa RUWASA, TARURA na watendaji wa Serikali za vijijini na kwenda kutatua kero hizo.
Aidha RC amewaagiza wakandarasi wanaokarabati au kutengeneza
Barabara kuhakikisha hawakati miti pasipokuwa na sababu kwa kuwa Mkoa upo katika
utekelezaji wa kampeni ya kupanda miti na utunzaji wa mazingira ikiwa ni maelezo
baada kuwasilishwa kwa kero ya ukataji miti ambayo haipo kwenye Barabara.
Hata hivyo Serukamba amewataka viongozi wa Serikali kwenye kata na vijiji wahakikishe wanawasikiliza wananchi na kutatua kero zao badala ya kukaa ofsini huku akiendelea kuonya tabia za watu unaowanyanyasa wanawake kwa kuwanyima haki ya kumiliki ardhi.
Aidha, ameonya tabia za wafugaji kuchunga kwenye mashamba ya watu huku akizitaka kamati za vijiji kuangalia mabwawa ya kunyweshea maji na kuweka mkakati wa mifugo kutopita kwenye mashamba ya wakulima ikiwa ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji kwa kupanda miti.
Zoezi la usikilizaji wa kero kwa mwezi Mei linaendelea kesho
katika Wilaya ya Manyoni
No comments:
Post a Comment