Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amelipongeza shirika lisilo la Kiserikali la Trees for the Future kwa kusimamia upandaji wa miti 15,358,918 katika Wilaya za iramba, Mkalama, Singida na Ikungi kupitia mradi wa bustani msitu.
Amesema shirika hilo lingesaidia kwa kiasi kikubwa kwa kubadilisha mazingira ya mkoa na kusaidia upatikanaji wa vipato kwa wakulima wadogo wadogo.
Akiongea wakati wa mahafali ya wakulima wapatao 249 wanaowakilisha wenzao 1445 waliohitimu mafunzo na utekelezaji wa mradi wa bustani msitu amesema kwa sasa wakulima hao huweza kunufaika kwa kuwa na misiti ambapo yapo mashirika ambayo yanalipa kwa uwepo wa misitu inayopunguza hewa ya ukaa.
RC ameahidi kwamba Serikali itatoa ushirikiano kwa shirika hilo kwa kuwa limeonesha dhamira ya dhati ya kuimarisha usalama wa chakula na lishe kwa wananchi wa Singida, kuinua kipato cha wakulima wadogo na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kupanda miti.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Nchini, Heri Rashid akielezea mradi huo amesema hadi sasa umezalisha vikundi vya wakulima vya huduma ya kuweka na kukopa vipatavyo 107 ambavyo vimesajiliwa katika Halmashauri za Singida, Mkalama, Iramba na Ikungi ili kuwasaidia wakulima kuweka na kukopa.
Aidha Heri ameeleza lengo la Shirika hilo kuwa ni kupanda miti Bilioni moja ifikapo mwaka 2030
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment