MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameiagiza Taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani hapo kuchunguza uhalali wa
fedha wanazotozwa wafanya biashara wa Soko la vitunguu Misuna lililopo kata ya
Misuna katika Manispaa ya Singida na
kuwachukulia hatua wote watakao bainika kuchukua fedha kinyume na utaratibu.
Serukamba ameyasema hayo alipotembelea soko hilo na
kusikiliza kero za wafanya biashara ambapo wengi walilalamikia kutozwa sh.200
kwa kila gunia la vitunguu, kila wiki washusha mizigo hutoa 5000, kila gari
likiangia linachajiwa 10,000 na madalali kutoa 2,000 fedha zote hizo hakuna
risiti inayotolewa huku wakiendelea kutoa ushuru wa soko hilo.
Amesema utaratibu ni kwamba kila fedha inayotolewa lazima
mtoaji apewe risiti vinginevyo zinapotelea kwenye mifuko ya watu hivyo
kuwaagiza TAKUKURU kuchunguza kama kuna jinai wawachukulie hatua huku akiitaka
taasisi hiyo kujikita zaidi kwenye kuzuia zaidi ili hali hiyo isiendelee.
Malalamiko mengine ni ukosefu wa miundombinu ya soko kama
uzio, uchafu kutozolewa kwa wakati hivyo kusababisha harufu kali na
kukosekana kivuli au vizuizi vya mvua au
jua jambo ambolo RC Serukamba alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuanza kufunika
eneo hilo kwa awamu na kazi hiyo ianze kabla ya mwezi wa Saba.
Hata hivyo Mkuu wa
Mkoa huyo amepiga marufuku wafanya biashara kutozwa ushuru mara mbili ndani ya
Mkoa mmoja na kuwataka Wakuu wa Wilaya
kulisimamia kwa kuwa watakaoumia ni
wakulima.
Marufuku hiyo imetokana na malalamiko ya wafanya biashara
kulalamikia mageti ya Manyoni na
Kintinku ambapo wamesema wanapoteza muda mrefu kwa ukaguzi ambao
unafanyika sokoni na vibali wamepewa.
Aidha Serukamba amesema atawasiliana na Mamlaka husika ili
kuhakikisha nchi nzima wanakuwa na kipimo cha gunia la vitunguu unaofanana ili kuleta
ushindani sawa.
"Haiwezekani Singida tunajaza gunia kwa vipimo vya
Serikali ambapo tunapinga rumbesa lakini maeneo mengine wanaachwa hii haileti
ushindani sokoni' Alisema Serukamba.
RC Serukamba ametoa wito kwa wafanyabiashara kufuata sheria
kanuni na taratibu katika biashara zao ili kuondoa changamoto ambazo
zinawakabili maeneo mbalimbali.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mheshimiwa Yagi Kiaratu akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa Soko la Vitunguu mkoani Singida Iddy Mwanja akizungumza wakati wakati Mkuu wa Mkoa wa Singida alipotembelea soko.
No comments:
Post a Comment