Thursday, March 30, 2023

RC Serukamba atoa maagizo kwa Wakurugenzi wakati wa Mafunzo ya mfumo wa Mshitiri

 

Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Singida wametakiwa kusimamia kikamilifu afua za mfumo wa ugavi wa bidhaa za Afya ikiwemo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa dawa (Medicine Audit) katika vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya kupunguza changamoto zinazotokana na usimamizi usioridhisha wa bidhaa hizo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba alipokuwa akifungua Mafunzo ya wawezeshaji wa mfumo wa Mshitiri yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo ambapo walijifunza namna ya utekelezaji wa mifumo wa mshitiri (Prime Vendor System).

Aidha amewataka kuongeza usimamizi wa ukusanyaji mapato katika vituo vya kutolea huduma za Afya ili viweze kulipa washitiri kwa wakati mara baada ya kupokea sheena ya bidhaa na kuepusha madeni yasiyokuwa ya lazima.

Kwa upande wake Emanuel Mayunga muwezeshaji wa ngazi ya taifa amesema kwamba mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi na kutekelezwa na Shirika la Swiss Tropical and Public Health Institute.

Aidha ameeleza kwamba mafunzo hayo ya mfumo mshitiri ambao yatasaidia katika uwezeshaji wa bidhaa za Afya zinazokuwa zimekosekana Bohari ya Dawa (MSD), hivyo kuimarisha na kurahisiha upatikanaji wa Bidhaa za Afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kupata wawezeshaji wa Mkoa na Halmashauri (T.O.Ts) wa Mfumo wa Mshitiri ambao wataenda kufundisha na kuwasimamia watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha katika mafunzo washiriki wamewezeshwa utekelezaji wa Mfumo wa Mshitiri (Prime Vendor System) kwa kupitia Mwongozo wa Utekelezaji wa Mfumo wa Mshitiri (Prime Vendor System Implementation Manual) pamoja na mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa taarifa za Mshitiri (Prime Vendor Management Information System).

Naye Elikana Lubango Mfamasia wa Mkoa  ameeleza kwamba katika ngazi ya Mkoa imeshapata washitiri wawili wanaofahamika kwa jina la Umoja na mwingine ni Serengeti wakiwa ni washitiri wa madawa na vifaa tiba.

MATUKIO KATIKA PICHA

Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Victorina Ludovick akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa kufungua rasmi mafunzo hao.


Mwezeshaji wa ngazi ya taifa Emmanuel Mhembano, ambaye pia ni Afisa TEHAMA Mkoa wa Singida akitoa mafunzo kwa washiriki.

Mwezeshaji wa ngazi ya taifa  Emanuel Mayunga  akitoa mafunzo kwa washiriki.

Elikana Lubango Mfamasia wa Mkoa  akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Baadhi ya Waganga Wakuu wa Wilaya za Halmashauri Mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment